1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 70 wauawa Islamabad

16 Julai 2007

Zaidi ya watu 70 wamepoteza maisha yao kufuatia mashambulio ya mabomu ya kujilipua mhanga yaliyotokea mwishoni mwa wiki nchini Pakistan.Kwa mujibu wa polisi mashambulio hayo yalitokea baada ya wapiganaji wa kiislamu kutoa wito wa vita vilivyo na misingi ya kidini kufuatia uvamizi wa msikiti ulio na msimamo mkali wa Taleban.

https://p.dw.com/p/CB2o
Rais Musharraf wa Pakistan
Rais Musharraf wa PakistanPicha: AP

Takriban watu 26 wakiwemo polisi 13 waliuawa hapo jana baada ya mlipuko kutokea kwenye kituo cha kusajili polisi katika mkoa wa kaskazini.

Watu 24 waliuawa na wengine kujeruhiwa siku ya jumamosi pale msafara wa kijeshi uliposhambuliwa katika eneo lililo kaskazini mwa Waziristan.

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao inatarajiwa kuongezeka.Rais pervez Musharraf wa Pakistan amelaani vitendo hivyo na kusisitiza kuwa serikali pamoja na raia wote wanapaswa kushirikiana kuondoa ugaidi nchini humo.

Umwagikaji huo wa damu unatokea baada ya wafuasi walio na msimamo mkali kwenye msikiti wa Lal ulioko mjini Islamad kupinga uvamizi.Jeshi la serikali lilivamia msikiti huo wiki jana na kusababisha vifo vya watu 86 wengi wao wapiganaji.Hili ni tukio baya zaidi kutokea nchini Pakistan tangu Rais Musharraf kuingia madarakani mwaka ‘99.