1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadha bado wamefungwa, lasema Amnesty International.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYce

Yangoon.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema kuwa kiasi cha waandamanaji 40 nchini Burma , ikiwa ni pamoja na watawa saba wa Kibudha, wamepewa hukumu ya kwenda jela katika kesi zilizoendeshwa kwa siri kuhusiana na maandamano ya mwaka jana ya kudai demokrasia.

Mwezi Septemba , watawa wa Kibudha waliongoza maandamano makubwa dhidi ya serikali mjini Yangon katika maandamano ambayo hayajaonekana katika muda wa miaka 20, lakini utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ulikandamiza kwa nguvu kubwa harakati hizo.

Inafahamika rasmi kuwa zaidi ya watu 3,000 wamekamatwa wakati wa msako huo. Utawala huo wa kijeshi umesema kuwa wengi wa waandamanaji wameachiwa huru, lakini Amnesty International imesema leo kuwa kiasi cha watu 700 bado wako kizuizini. Kundi hilo la kutetea haki za binadamu limeitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimizo linaakisi wasi wasi wa jumuiya ya kimataifa kuhusiana na uendeaji kinyume haki za binadamu nchini Burma.