1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu kadha wakamatwa kwa kufanya ghasia.

16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcDp

Hamburg.

Polisi katika mji wa kaskazini nchini Ujerumani wa Hamburg wamewakamata zaidi ya watu 60 kufuatia ghasia katika moja kati ya mitaa maafuru yenye maduka. Watu walioshuhudia wamesema kuwa makundi ya watu waharibifu yalianza ghasia baada ya maandamano ya wanaharakati wa mrengo wa shoto wapatao 3,000 , ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani. Waandamanaji walikuwa wakiandamana kupinga kile wanachokieleza kuwa ni hali ya serikali kuzama mno katika fikira za kiusalama nchini humo.