1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu mashuhuri na miaka 60 ya DW

23 Aprili 2013

Machozi yangu yote namalizikaa..Miye nitalala na nani we unaendaa.. Mimi ni Papa Wemba. Bakaladi Yakuba. Nimesikiliza DW.“ Papa Wemba, Mwanamuziki Maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

https://p.dw.com/p/18LAE
Papa Wemba aus Kongo, der König des Rumba-Rock, ist einer der Superstars des Africa-Festivals 2011, des größten Festivals für afrikanische Musik in Europa Foto: Carine Debrabandère, Würzburg, Juni 2011
Papa WembaPicha: DW

"Ningependa kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Deutsche Welle kwa kazi nzuri munayoifanya ya kukikuza Kiswahili kwamba ni katika miongoni mwa redio za mwanzo kutumia Kiswahili. Katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kat, Deutsche Welle imekuwa na umaarufu mkubwa sana. Kupitia kwenu, hata wale ambao Kiswahili si lugha yao ya kwanza wameweza kujifunza mengi. Pia mumekuwa wawazi kutangaza matukio mbali mbali yanayotokea hasa pale unapotokea ukandamiazaji wa haki za wananchi, penye dalili ya uimla au udikteta mumekuwa hamutafuni maneno.“ - Maalim Seif Sharif Hamad, Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar.

CUF’s Sansibar Präsidentschaftskandidat, Seif Sharif Hamad, beim Gespräch mit Journalisten, nachdem der das Formular für seine Kandidatur bei der Sansibar Wahlkommission (ZEC) abholte (5.Juni 2010) Stichwort: Sansibars Präsidentschaftskandidat, Zanzibar Presidential Candidate, Seif Sharif Hamad
Makamo wa rais Zanzibar, Seif Sharif HamadPicha: DW

“Kituo chetu kinafanya kazi vizuri na Deutsche Welle hasa Idhaa ya Kiswahili kwa sababu Watanzania wengi tunaongea Kiswahili kwa hiyo watu wanasikiliza Kiswahili. DW inatoa taarifa ambazo zinasambaa nchi nzima. Tumekuwa tukipokea taarifa na watu wamekuwa wakituambia taarifa hii nimeisikia DW wengine wamekuwa wakituambia kwa kusikiliza DW tumekuwa tukiwasikia ninyi na kusikia taarifa mbali mbali, kwahiyo DW imekuwa ni nzuri sana au ni sauti ambayo sisi ambao tunazungumza mambo ya kuwafikia watu na watu kuweza kuzungumza masuala yao kupitia redio hii.” - Helen Kijo Bisimba, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania.

Helen Kijo-Bisimba, Direktorin der Menschenrechtsorganisation Legal and Human Rights Centre (LHRC) in Daressalam *** Bilder Deutsche Welle, Julia Hahn, November 2012 Ort: Daressalam, Tansania *** http://en.wikipedia.org/wiki/North_Mara_Gold_Mine North Mara Gold Mine is an open pit gold mine in the Tarime District of the Mara Region of Tanzania. It is operated by African Barrick Gold. It is one of four gold mines African Barrick Gold, a subsidiary of Barrick Gold, operates in Tanzania, the other three being Tulawaka, Bulyanhulu and the Buzwagi Gold Mine. In the financial year 2009, the four operations produced a combined amount of 716,000 attributable ounces of gold.
Mkurugenzi wa Kituo cha Hki za Binaadamu Tanzania Helen Kijo-BisimbaPicha: DW/J. Hahn

“Mimi nimeanza kuisikiliza Deutsche Welle kwa muda mrefu sana, miaka ya ‘60 nikiwa mwanafunzi wa shule za msingi nilikuwa namsikia baba anafungua DW wakati nikiwa sekondari hata nikiwa Chuo Kikuu Dar es Salaam nilikua napenda sana kusikiliza redio yenu. Uzuri wa taarifa ya habari na matangazo mengine yanayotoka kwenye DW ni kwamba ni ya uhakika ambayo mtu akiyasikiliza hawi na wasi wasi. Kwa hiyo ni redio yenye heshima na sifa kubwa sana nchini mwetu na pembe nyengine za Afrika.” - Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini Tanzania

Sospeter Muhongo, Minister für Energie und Mineralien in seinem Büro *** Bilder Deutsche Welle, Julia Hahn, November 2012 Ort: Ministry of Energy and Minerals, Daressalam, Tansania *** http://en.wikipedia.org/wiki/North_Mara_Gold_Mine North Mara Gold Mine is an open pit gold mine in the Tarime District of the Mara Region of Tanzania. It is operated by African Barrick Gold. It is one of four gold mines African Barrick Gold, a subsidiary of Barrick Gold, operates in Tanzania, the other three being Tulawaka, Bulyanhulu and the Buzwagi Gold Mine. In the financial year 2009, the four operations produced a combined amount of 716,000 attributable ounces of gold.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter MuhongoPicha: DW/J. Hahn

"DW imekuwa ni chombo kinachounganisha sauti zetu. Unajua vyombo vya habari vinasaidia kueleza kuwafahamu watu wa nchi mbali mbali kwa hiyo mumekuwa mukiunga bara la Afrika na sehemu nyingine duniani. Tumepata fursa ya kufahamu mambo yanayotokea sehemu mbali mbali. Ya pili ni Kiswahili. Nataka niwapongeze kwa hilo kuweka lugha ya Kiswahili na kuitumia kwa kuwaelewesha wazungumzaji wa Kiswahili. Mimi nadhani hiyo ni kati ya vitu ningependa kuwapongeza.“ - Getrude Mongella, Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika.

“Naipongeza DW. Naona ni nafasi adhimu kwa Idhaa ya Kimaifa kutangaza kwa lugha nyingi za kando. Kwa sababu kama mimi najifunza pia tamaduni za lugha nyengine. Hivyo ni muhimu kuona kuwa hata tamaduni za jamii tofauti zinazingatiwa, mawasiliano yanafika hadi kwenye ngazi za chini na matumaini ya wasikilizaji yanatimizwa na hivyo DW inafanya kazi kubwa kwa ajili yetu.“ - Auma Obama, Dada wa Rais Barack Obama wa Marekani.

Dr. Auma Obama, Kenier, Initiatorin und Vorsitzende der Jugendinitiative und Stiftung "SautiKuu - powerful Voices for a powerful youth" in Kenia. Sie ist die Halbschwester des US-Präsidenten Barack Obama, hat in Deutschland studiert (Heidelberg und Bayreuth) und in England gearbeitet, bevor sie nach Kenia zurückkehrte. Aufnahme: 27.11.2012, Bonn, Foto: Helle Jeppesen für DW
Dk. Auma Obama Dada wa rais Barack ObamaPicha: DW/ H. Jeppesen

“Hongereni sana maana munatusaidia sana kueneza sifa ya Kiswahili duniani na Kiswahili ni lugha moja ambayo inakuwa zaidi ya lugha nyingi duniani. Hivi karibuni kwa kweli Kiswahili kitakuwa lugha moja ya dunia ikishindana na lugha nyengine, kama vile Kiingereza, Kitaliana au Kihispania.“ - Prof. Ngugi wa Thiong'o, Mwandishi na Mhadhiri wa Fasihi kutoka Kenya.

Der kenianische Autor Ngugi wa Thiong'o Es handelt sich um ein Bild des Autors und seines Romans/bzw das Buchcover. Die Fotos konnte ich von der Presseseite des A1-Verlages zu weiteren journalistischen Verwendung frei herunterladen. Zulieferer: Ralf Bosen Eingestellt November 2010
Mwandishi wa vitabu wa Kenya Ngugi wa Thiong'oPicha: A1 Verlag

“Deutsche Welle ni redio ambayo mimi mwenyewe nimekuwa naisikiliza tangu nikiwa mdogo sana, tangu nikiwa shule ya sekondari,sio tu kwa sababu ya unadhifu wa lugha inayotumika yaani Kiswahili. DW imetoa mfano kwamba katikati ya bara la Ulaya kuna redio inazungumza Kiswahili na kusikika katika maeneo mengi sana. Sasa hivi sio nchi za Afrika ya Mashariki lakini hata Afrika ya Kati. Mimi mwenyewe nimekuwa Rwanda nimekuwa Congo nimeweza kusikiliza DW. Muendelee na tunawatakia kila la heri na muongeze vipindi ambavyo vitarutubisha lugha yetu ya kiswahili na wasikilizaji waongezeke zaidi na zaidi.“ - Balozi Augustine Mahiga, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia. Sikiliza sauti za baadhi ya watu hao kwa kubonyeza kitufe cha alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi