1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu tisa wauawa katika shambulio la Munich

23 Julai 2016

Kiasi watu wanane wameuwawa katika shambulio la kigaidi la risasi mjini Munich, polisi imesema usiku wa Ijumaa (22.07.2016)

https://p.dw.com/p/1JUbv
Deutschland Polizisten sichern nach einer Schießerei das Gelände
Polisi wakiwasaka washambuliaji mjini MunichPicha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Polisi imeongeza kwamba mwili wa tisa uliopatikana karibu na eneo la tukio na huenda ni mmoja kati ya washambuliaji, lakini wenzake bado hawajulikani waliko.

Polisi wamezungumzia kuhusu "hali mbaya ya kigaidi" katika mji huo wa kusini mwa Ujerumani baada ya mashambulizi ya risasi katika eneo la maduka la Olimpia na kusababisha polisi kuwaondoa watu kutoka katika eneo hilo na hali ya mtafaruku mkubwa katika mji huo.

Uchunguzi wa mwili wa mtu wa tisa , uliopatikana kiasi ya kilometa moja kutoka katika kituo hicho cha maduka , unaonesha alifariki katika hali ya mapambano, polisi wamesema.

Deutschland Olympia Einkaufszentrum in München Hauptbahnhof Polizei
Gari la kubebea wagonjwa likiwasafirisha majeruhi na waliouwawaPicha: Getty Images/J. Koch

Maafisa mjini Munich wamekiweka tayari kikosi cha kupambana na ugaidi cha GSG 9 na kuomba wanajeshi zaidi kuimarishwa kikosi hicho na polisi zaidi kutoka sehemu nyingine nchini humo.

Hakujakuwa na tukio lingine la kigaidi mjini Munich, polisi imesema, ikikanusha ripoti za vyombo vya habari nchini Ujerumani kwamba kulikuwa na tukio jingine la mapambano katika eneo la Karlsplatz, ambalo pia linafahamika kama Stachus, karibu na eneo la kati la mji huo na kiasi ya kilometa tano kutoka eneo la maduka la Olimpia.

Mwandish: Sekione Kitojo / dpae