1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wasiopungua 12 wauawa katika vurugu za kijamii Nigeria

Iddi Ssessanga
9 Januari 2018

Zaidi ya watu 10 wameuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano yanayodhihirisha kuwa ya kulipizana kisasi kati ya wakulima na wafugaji nchini Nigeria, zimesema duru za polisi na jamii.

https://p.dw.com/p/2qYf3
Zentralafrikanische RepublikTrauer in Bangui
Picha: Getty Images/AFP/E. Dropsy

Msemaji wa polisi David Misal alisema watu 12 waliuawa wakati watu wasiotambulika waliokuwa na silaha waliposhambulia kijiji cha kabila la Fulani siku ya Ijumaa.

Shambulizi la kulipiza kisasi lilifuatia siku ya Jumamosi, aliongeza. Wakaazi wa vijiji vilivyoathirika walisema idadi ya waliokufa ni 40, lakini idadi hii haikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Mashambulizi hayo ndiyo ya hivi karibuni katika mgogoro wa muda mrefu wa umuagaji damu kuhusiana na ardhi, unaopaliliwa na migogoro ya kidini na kikabila, ambao umesababisha vifo vya maelfu katika miongo ya karibuni.

Kundi la kimataifa linalojihusisha na utatuzi wa migogoro la ICG, lilionya Septemba iliyopita kwamba mgogoro huo ulikuwa unaanza hatari kama uasi wa kundi la Boko Haram kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Niger Normaden Fulani Scharfherde bei Gadabeji
Mfugaji wa kabila la Fulani akichunga ng'ombe wake. Picha: AP

Mfugaji Abdullahi Hamma alisema wanaume kutoka kijiji kinachokaliwa na watu wengi wa kabila la Bachama walifanya shamulizi majira ya alfajiri kwenye kijiji chake cha Donadda na vingine viwili, Babagasa na Katibu. "Tulizika watu 15 waliouawa katika mashambulizi dhidi ya jamii zetu," aliongeza.

Siku ya Jumamosi, wafugaji wa kabila la Fulani walivamia kijiji cha Wabachama cha Robi wakiwa kwenye pikipiki na kuwafyatulia risasi wakaazi. "Tulipoteza watu 25 katika shambulizi ambalo halikuchokozwa lililofanywa na washambuliaji wa Fulani dhidi ya kijiji chetu," alisema kiongozi wa vijana katika kijiji cha Robi Felix Uban-Doma. "Watu kadhaa walijeruhiwa.

Mashambulizi ya kuvuka mipaka ya majimbo

Msemaji wa polisi Misal alisema hayo yalikuwa ziada ya vurugu sawa zilizotokea mwzi uliyopita katika jimbo jirani la Adamawa. Wilaya ya Lau iko karibu na mpaka wa jimbo hilo.

Wakati huo, wafugaji wasiopungua 30 wa kabila Fulani waliuawa na wapiganaji wa Bachama katika mashambulizi dhidi ya vijiji vinne vya Wafulani katika wilaya ya Numan ya jimbo hilo.

Mauaji hayo yalisababisha kisasi kutoka kwa Wafulani kwenye vijiji vya karibu vya Bachama ambako watu kadhaa waliuawa, na kusababisha uhamaji mkubwa wa tu kutoka eneo hilo.

"Ni wale walioathirika na shambulio dhidi ya ndugu zao wilayani Numan waliozishambulia jamii za Fulani wilayani Lau, ambayo inashiriki mpaka na jimbo la Adamawa na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi," alisema Misal.

Polisi walipelekwa katika maeneo yalioathirika ili kuzima vurugu hizo, alisema Misal, na kuongeza kuwa polisi waliwakamata washukiwa wawili kuhusiana na vurugu hizo.

Nigeria Konflikte
Wanawake na watoto wakipanga foreni kuchota maji mtoni baada ya mashamblizi ya Fulani katika jimbo la Beneue.Picha: Getty Images/AFP/E. Arewa

Rais Buhari alaani mashambulizi hayo

Watu wengine kadhaa wanaaminika kuuawa katika wiki ya vurugu kati ya wafugaji wa Fulani na wakulima wa kabila la Tiv katika maeneo ya Guma na Logo yalioko katika jimbo la Central Benue. Msemaji wa polisi ya Benue Moses Joel Yamu alisema bado haijabainika wazi ni watu wangapi waliuawa.

Jumatano iliyopita, mamia ya waandamanaji waliingia mitaani katika mji mkuu wa jimbo la Banue, Makurdi, kupinga mashambulizi  dhidi ya jamii za wakulima.

Rais Muhammadu Buhari - Mfulani anaezungumza Kihaussa kutoka Kaskazini mwa Nigeria, amelaani mapambano hayo yanayosababisha umuagaji damu ambayo aliyataja kuwa ya kiovu na sugu."

Mwandishi: Iddi Ssessanga/afpe

Mhariri: Saumu Yusuf