1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Watu watatu wauawa na Al-Shabaab katika hoteli ya Mogadishu

Sylvia Mwehozi
15 Machi 2024

Watu watatu wameuawa katika makabiliano ya risasi yaliyodumu kwa muda baina ya wanamgambo wa Al-shabaab na maafisa wa usalama katika hoteli moja maarufu karibu na makazi ya rais kwenye mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu.

https://p.dw.com/p/4dgKR
Somalia | Al-Shabaab
Al shabaab wameshambulia katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kusababisha mauaji ya watu watatuPicha: Feisal Omar/REUTERS

Msemaji wa polisi Kanali  Qasim Ahmed Roble amewaeleza waandishi wa habari kuwa watu wengine 27 wamejeruhiwa wakiwemo raia 18 na askari 9. Maafisa wa usalama pia waliwaua wanamgambo watano wakati wa makabiliano ya kutumia bunduki.

Wapiganaji wenye silaha waliivamia hoteli ya SYL na kufyetua ovyo risasi usiku wa jana, kabla ya vikosi vya usalama kutangaza leo ijumaa kwamba wamerejesha utulivu baada ya saa 13 za mzingiro.

Wanagambo wa Al Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara na kusababisha maafa

Shambulio hilo dhidi ya hoteli ya SYL, ambayo imelengwa mara kadhaa kipindi cha nyuma limetokea mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, jambo ambalo ni la nadra kufanywa na wanamgambo wa Al Shabaab.