1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wamekufa kwa kipindupindu Burundi

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZox

BUJUMBURA

Watu wawili wamekufa kutokana na kuzuka upya kwa ugonjwa wa kipindupindu kusini mashariki mwa Burundi.

Kwa mujibu wa afisa wa serikali ya mtaa Epimene Batsinda watu wawili wamekufa kutokana na kipindupindu hicho hapo jana na wengine 57 wamelazwa hospitalini katika kituo cha afya cha Ziwa Nyanza kilioko kilomita 130 kutoka Bujumbura.

Amesema takriban watu 151 wameambukizwa ugonjwa huo tokea kuripuka kwake kwa mara ya kwanza hapo Desemba Mosi.

Ameongeza kusema kwamba mripuko wa kipindupindu hutokea mara kwa mara katika mji wa Ziwa Nyanza wenye wakaazi 54,000 kutokana na Ziwa Tangayika kuwa njia pekee ya kujipatia maji ya kunywa na pia kudhibiti afya kwa kuondowa maji taka.