1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watuhumiwa wa mashambulio ya kigaidi wafikishwa mahakamani mjini Madrid leo

15 Februari 2007

Hatua za usalama zimeimarishwa mjini Madrid leo ambapo watuhumiwa 29 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kuhusiana na mashambilio ya mabomu yaliyoua watu 191 katika treni mwaka 2004 nchini Uhispania.

https://p.dw.com/p/CHK5
Mashambulio ya kigaidi mjini Madrid
Mashambulio ya kigaidi mjini MadridPicha: AP

Watuhumiwa wakuu katika keshi hiyo, wengi wao wakiwa na nasaba za Kimorocco wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji na wanaweza kupewa adhabu ya vifungo vya hadi miaka 30 jela ikiwa watapatikana na hatia.

Watuhimiwa wengine wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama za kushirikiana na magaidi na kusaidia katika upatikanaji wa silaha.

Katika mashambulio hayo ya mabomu ndani ya treni watu 191 waliuawa katika mji wa Madrid mnamo mwaka 2004.Watu wengine alfu moja na mia saba walijeruhiwa.

Magaidi walifanya mashambulio hayo wakati ambapo palikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanatumia usafiri wa treni.

Maafisa wa idara ya upelelezi wamewalaumu magaidi wa mtandao wa alkaida kanda ya Uhispania kwa kufanya unyama huo.

Kingozi wa kundi hilo la magaidi Serhene bin Abdelmajid anatoka Tunisia na wengine walioshirikiana nae wanatoka Algeria,Syria na Lebanon.

Abdu Mtullya