1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watumishi 6 wa Zoe's Ark wasukumwa jela miaka minane kila mmoja

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cyq7

PARIS:

Mahakama nchini Ufaransa imewahukumu wafanyakazi sita wa shirika moja la kimisaada la Ufaransa,Zoe’s Ark, kifungo cha miaka minane jela kila mmoja kwa kujaribu kuteka watoto 103 kutoka Chad mwaka jana. Watu hao sita walirejeshwa nyumbani Ufaransa mwaka jana baada ya serikali za Ufaransa na Chad kufikia makubaliano ya kuwataka watekeleze kifungo chao nchini Ufaransa. Walihukumiwa kwenda jela kwa miaka minane na kazi ngumu nchini Chad hukumu iliozusha hamasa.Shirika la Zoe’s Ark linasema watoto hao walikuwa yatima kutoka Darfur.