1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watumishi wa Deutsche Welle...

23 Aprili 2013

...wanasimulia kile walichokishuhudia tangu walipojiunga na DW, kuanzia enzi za matangazo kupitia vipimo vya masafa mafupi hadi kuingia katika enzi za mtandao.

https://p.dw.com/p/18HWO
Ying Dai anafanyakazi na idhaa ya kichina ya DWPicha: DW

Ying Dai

Ninakumbuka vizuri mwanzoni mwa enzi za mtandao Deutsche Welle. Wakati ule, miaka 15 iliyopita, tulikuwa tukitoa katika diski ripoti ambayo tayari ilikuwa imeshaandikwa na baadae kuwapelekea diski hiyo wenzetu wa idara ya teknolojia ya mawasiliano-IT, walioko katika ghorofa ya tano. Wao ndio waliokuwa wakishughulika na yaliyosalia.

Hivi sasa tunatayarisha wenyewe kila kitu na kila siku kupitia mfumo wa mchanganyiko wa vyombo vya mawasiliano ya kimambo leo katika jengo leo la kimambo leo la Radio. Naiwe picha au ripoti, naiwe sauti au video- yote hayo tunaweza hivi sasa kuyatayarisha wenyewe.

Nilipoanza kazi na Deutsche Welle mnamo mwaka 1996, vipimo vya mwimbi mafupi ndio njia pekee tuliyokuwa nayo kueneza matangazo yetu. Tangu wakati huo njia za kueneza habari zimeongezeka na kuimarika. Nina fahari ya kupata fursa ya kujionea mwenyewe mageuzi haya. Kwasababu ni wale tu walio tayari kujifunza mepya tu ndio wasiozeeka na wanaoendelea kujisikia vizuri. Kwa maoni yangu, miaka 60 baadae, Deutsche Welle bado inalingana na wakati kwasababu Deutsche Welle daima inakwenda na wakati.

Lavinia Pitu

DW 60 Jahre Mitarbeiter Statements Lavinia Pitu
Lavinia Pitu anafanyakazi na idhaa ya kirumaniaPicha: DW

Hadithi ya kusisimua na ya kuchekesha ninayoikumbuka inamhusu mjasiriamali mmoja kijana kutoka Berlin, Cantemir Gheorghiu, anaetokea Rumania anaenitaja kuwa mie ndie niliyemvumbua. Kwanini? Kwasababu yeye amevumbua miwani ya mabango. Miwani ya fesheni aliyotengeneza kwa mabango na kuiuza katika soko la vitu vya zamani. Mwaka 2010 niliandika ripoti mbili au tatu kuhusu mada hiyo kwaajili ya mtandao wa idhaa ya kiingereza na kirumania na pia kwaajili ya matangazo ya radio.Wiki mbili au tatu baadae waandishi habari kutoka Berlin na pia kutoka Rumania wakamjia. Imekwenda kwendaje hata akapata fikra ya kutengeneza miwani ya mabango? Ilitokezea siku moja usiku alitengeneza miwani kwa kutumia mabango na akaenda nayo baa. Muuzaji wa baa hiyo akataka kuinunua miwani hiyo. Hapo ndipo alipopata fikra ya kufanya biashara ya miwani hiyo. Hivi sasa amefungua biashara kubwa ya miwani, anauza miwani hizo barani Asia na kila mahala barani Ulaya na anasema: "Ndio nimefanikiwa kwasababu wewe ndiye uliyeripoti kuhusu miwani zangu."

Renate Krieger

DW 60 Jahre Renate Krieger portugiesisches Programm
Renate Krieger wa idhaa ya kirenoPicha: DW

Kuwa karibu zaidi na wasikilizaji wangu ndio muhimu zaidi kwangu mimi. Nimeitambua hali hiyo kwa mara ya mwanzo tulipoanza kujibu masuala kupitia SMS na mtandao wa kijamii wa Facebook. Kila siku tunauliza masuala na tunapokea majibu mengi sana kutoka kwa wasikilizaji wetu. Hata katika maeneo tunayoyatangazia, hali hiyo nimeishuhudia. Nchini Angola kwa mfano, watu wamekitambua kikuza sauti. Nchini Senegal pia nilikokwenda kuripoti kuhusu kongamano la kimataifa la kijamii. Na kutoka Guinea-Bissau, nimeambiwa kwamba wasikilizaji wanawajua kwa majina wafanyakazi wote wa idhaa yetu. Wanajua vizuri nani nahodha wa matangazo ya usiku. Mmoja wetu akipelekwa katika eneo tunalolitangazia, wasikilizaji wanakuwa wanatuuliza pia. Ninafurahi kusikia. Kwasababu ninapokuwa hapa studio na kuona vifungo vyote hivi, ninatambua kwamba upande wa pili kuna watu wanaosubiri kusikiliza ripoti zetu.

Mwandishi:Drechsel, Alexander/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman