1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waturuki wapiga kura ya maoni ya kihistoria

16 Aprili 2017

Kura zimeanza kuhesabiwa baada ya kura ya maoni iliofanyika Jumapili (16.04.2017) ambayo itampa madaraka makubwa Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki na kuanzisha mabadiliko makubwa sana ya mfumo wa kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/2bJwG
Türkei Referendum Auszählung in Gaziantep
Picha: picture alliance/AA/K. Kocalar

Vituo vya kupigia kura vimefungwa nchini kote saa kumi na moja jioni na matokeo yanatarajiwa kutolewa wakati wowote ule.Vituo vya mashariki ya Uturuki ambavyo vilifunguliwa mapema kwa saa moja vilifungwa saa kumi jioni.

Uchunguzi wa maoni ulionyesha kura za "Ndio" zilikuwa zinaongoza kwa tofauti ndogo jambo ambalo litabadili demokrasia inayotumika bungeni kwa kumpa madaraka makubwa Rais Tayyip Edogan ambaye yumkini akabakia madarakani angalau hadi mwaka 2029.

Matokeo hayo yatajenga taswira mpya ya uhusiano kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya.Nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya Kujihami ya NATO imedhibiti wimbi la wahamiaji wengi wao wakiwa wakimbizi wanaokimbia vita kutoka Syria na Iraq kuingia katika nchi za umoja huo lakini Erdogan amesema yumkini akaagalia upya makubaliano yaliyofanikisha hayo baada ya kumalizika kwa kura hiyo ya maoni

Erdogan ashingiliwa

Türkei Referendum Wahllokal in Istanbul Präsident Erdogan
Rais Tayyip Erdogan na mkewe Emine wakipiga kura wakiandamana na wajukuu zao mjini Istanbul.Picha: Reuters/M. Sezer

Umma ilikuwa ukipiga mayowe ya "Recep Tayyib Erdogan " na kumshangiia wakati rais huyo alipokuwa akipeana mikono na kusalimiana na watu baada ya kupiga kura katika shule karibu na nyumbani kwake mjini Instanbul. Wafanyakazi wake walikuwa wakigawa vitu vya kuchezea kwa watoto.

Baada ya kupiga kura yake  Erdogan amesema katika kituo cha kupiga kura kwamba "Mungu akipenda anaamini wataamuwa kufunguwa njia kwa maendeleo zaidi ya haraka."

Amesema "Ninaamini busara ya kawaida waliyo nayo watu wengi kwa demokrasia."

Takriban watu milioni 55 wanastahiki kupiga kura katika vituo 167,140.Wapiga wa Kituruki walioko nje ya nchi tayari wamepiga kura zao.

Kura hiyo ya maoni imeligawa vibaya taifa. Erdogan na wafuasi wake wanasema mabadiliko yanahitajika kuirekebisha katika iliopo sasa iliyoandikwa na magenerali kufuatia mapinduzi ya mwaka 1980 ili kukabiliana na changamoto za usalama na kisiasa zinazoikabili taifa hilo na kuepuka serikali dhaifu za mseto zilizokuwepo zamani.

Utawala wa mtu mmoja

Türkei Referendum Wahllokal in Diyarbakır
Wananchi wakipiga kura Diyarbakir.Picha: picture alliance/AP Photo/E. Tazegul

Bayram Seker mwenye umri wa miaka 42 baada ya kupiga kura ya "Ndio" mjini Instanbul amesema "Hii ni fursa yetu kudhibiti tena nchi yetu"Ameongeza kusema "Sifikiri utawala wa mtu mmoja ni kitu cha kutisha na kwamba Uturuki huko nyuma iliwahi kutawaliwa na mtu mmoja" akimaanisha muasisi wa taifa ka kisasa la Uturuki Mustafa Kemal Atarurk.

Wapinzani wanasema hiyo ni hatua kuelelekea kwenye udikteta mkubwa katika nchi ambapo watu 47,000 wako magerezani wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao na wengine 120,000 wamefukuzwa au kusitishwa kazi kutokana na msako kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindwa mwezi wa Julai mwaka jana jambo lililozusha shutuma kutowa kwa washirika wake wa mataifa ya magharibi na mashirika ya haki za binaadamu.

Uhusiano kati ya Uturuki na Ulaya ulifikia kiwango cha chini wakati wa kampeni za kura hiyo ya maoni ambapo nchi za Umoja wa Ulaya ikiwemo Ujerumani na Uholanzi  ziliwapiga marufuku mawaziri wa Uturuki kufanya mikutano ya hadhara ya kuunga mkono mabadiliko hayo ya katiba.

Erdogan aliziita hatua hizo kuwa "Vitendo vya Wanazi" na kusema Uturuki itafikiria upya uhasiano wake na Umoja wa Ulaya baada ya miaka ya mingi ya kutaka kuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mwandishi : Mohamed Dahman/  Reuters

Mhariri: Isaac Gamba