1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wauguzi na daktari wasubiri hukumu ya mahakama Libya

Mohammed Abdul-Rahman10 Julai 2007

Mahakama nchini Libya inatarajiwa Jumatano kutoa hukumu yake kuhusiana na rufaa iliokatwa na wauguzi watano wa Kibulgaria na daktari mmoja wa Kipalestina, waliopatikana na hatia ya kuwaambukiza virusi vya ukimwi mamia ya watoto

https://p.dw.com/p/CHBC
Wauguzi watano wakibulgaria na daktari wa kipalestina wakiwa mahakamani
Wauguzi watano wakibulgaria na daktari wa kipalestina wakiwa mahakamaniPicha: AP

Uamuzi huo wa mahakama unatarajiwa wakati ambapo mazungumzo yamekua yakiendelea juu ya malipo ya fidia kwa familia za wahanga, suluhisho linalosakwa nje ya mahakama na ambalo linaweza kuwanusuru washitakiwa na adhabu ya kifo.

Washitakiwa hao ,wauguzi watano wakibulgaria na daktari mmoja wakipalestina ambaye sasa amepewa uraia wa Bulgaria wako ndani kwa mwaka wanane na walihukumiwa kifo miaka mitatui iliopita . wanashutumiwa kuwaweka damu iliokua na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi, jumla ya watoto 438 katika hospitali moja mjini Benghazi.

Licha ya kuhukumiwa kifo Mei 2004, washitakiwa hao wanashikilia kwamba hawana hatia, wakisema wamekiri makosa hayo kutokana na mateso. Wanasema miezi michache baada ya mkutiwa nguvuni Februari 1999, walipigwa, kuchomwa na wayai za umeme na kutishwa kwa kutumiwa umbwa na afisa mmoja wa polisi na mwenzake kutoka idara ya upelelezi ambao nao wamefungua mashitaka wakidai kuharibiwa sifa na kutaka walipwe fidia.Wataalamu wa kigeni wa masuala ya tiba , wamesema huenda ukosefu wa usafi wa kutosha ukawa sababu ya janga hilo lilotokea mjini Benghazi , mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

Kwa mujibu wa mwanasheria mmoja wa Kilibya Othman al-Bizanti anayewatetea wauguzi hao, huenda mahakama isiidhinishe hukumu hiyo kama ilivyofanya mwezi uliopita, ili ukweli halisi ufahamike na haki itendeke.

Miongoni mwa yale yanayozingatiwa ni hatimae maridhiano kuwasilishwa mbele ya baraza kuu la majaji ambalo huenda likaamua kubatilisha adhabu ya kifo na badala yake kuwa vifungo jela. Adhabu hiyo huenda ikatimizwa nchi wanakotoka washitakiwa. Libya na Bulgaria zina makubaliano ya kurudishiana wahalifu wa upande wa pili.

Umoja wa ulaya na wakfu wa Gaddafi ambayo ni jumuiaya ya misaada inayoongozwa na mtoto wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, wamefikia maridhiano juu ya kuwatunza watoto walio hai. Kwa mujibu wa msemaji wa familia za walioathirika Idriss Laghani kwamba kuna kikwazo kimoja tu kilichoasalia nacho ni suala la ulipaji fidia, akitumai kwamba maridhiano pia yatafikiwa katika suala hilo.

Umoja wa ulaya unaoamini kwamba washitakiwa hawana hatia yoyote umesisitiza mara kwa mara kwamba unapinga mbinu zozote za kushinikiza ulipaji fidia na badala yake unataka familia na wahanga wasaidiwa pamoja na kuboresha huduma za tiba katika hospitali hiyo ya Benghazi.

Libya kwa upande mwengine imeahidi pia kuboresha uhusiano wake na umoja wa Ulaya, baada afisa zamani wa upelelezi wa Libya Abdelbaset Ali Mohamed al Megrani, kukubaliwa kukata rufaa na kesi yake kusikilizwa upya. Megrani anatumikia kifungo nchini Uingereza kwa kuhusika katika mripuko wa bomu dhidi ya ndege ya abiria katika anga ya Lockerbie nchini Scotland 1998.