1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibada ya amani ya uchaguzi wa Zimbabwe

Sudi Mnette
21 Agosti 2023

Raia wa Zimbabwe wamefanya ibada ya kuiombea amani ikiwa kabla ya uchaguzi wa kitaifa wa Agosti 23 unaotarajiwa kuwa na mvutano mkubwa huku kukiwa ukandamizaji dhidi ya upinzani na mashaka ya wizi wa kura.

https://p.dw.com/p/4VO5k
Simbabwe | Straßenszene in Harare
Picha: Dan Kitwood/Getty Images

Idadi kubwa ya waumini ilikusanyika katika ibada ya Jumapili (20.08.2023) kwa ajili ya misa katika kanisa lililopo katika barabara isio na lami na kuzungukwa na vibanda vya soko katika kitongoji kikongwe zaidi cha jiji la Harare cha Mbare.

Mchungaji wa kanisa hilo lenye kufahamika kama Apostolic Faith Mission, Edson Mukaro amenukuliwa akisema "Tunaombea mazingira ya amani. "Tunawahimiza tu, watu wetu kuwa watulivu, amani, na kufanya kila kitu kwa utaratibu."

Zimbabwe na chaguzi zenye mizozo.

Simbabwe Wahlen l Anhänger der ZANU-PF des Präsidenten Mnangagwa
Wafuwasi wa chama tawala nchini Zimbabwe cha ZANU-PF wakiwa katika harakati za mwishonI za kampeni.Picha: Zinyange Auntony/AFP via Getty Images

Zimbabwe ina historia ndefu ya chaguzi zenye mzozo zilizokumbwa na ghasia, na baadhi wanahofia kurudiwa kile kilichotokea mwaka wa 2018,pale ambapo jeshi lilipowafyatulia risasi waandamanaji wa upinzani, na kusababisha vifo vya watu sita.

Siasa na dini mara nyingi hufungamana katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ambako makanisa ya yanatawala na rekodi zinaonesha baadhi ya viongozi wa kidini katika miaka ya nyuma waliegemea upande wa chama tawala cha ZANU-PF, ambacho kimekuwa katika hatamu ya uongozi tangu uhuru wa taifa hilo mwaka 1980.

Nelson Chamisa mpinzani ambae pia kiongozi wa kidini.

Simbabwe Wahlen l Nelson Chamisa, Citizens Coalition for Change (CCC)
Kiongozi wa Muungano wa Mabadiliko wa Zimababwe (CCC) Nelson Chamisa, akinadi sera zake kabla ya Agosti 23.Picha: Zinyange Auntony/AFP via Getty Images

Nelson Chamisa, mwenye umri wa miaka 45, ambae ni mpinzani mkuu wa Rais Emmerson Mnangagwa, ni mchungaji katika madhehebu ya "Apostolic", lakini katika kanisa lisilohusiana na la mchungaji Mukaro.

Mwenyewe Mukaro anasema jengo la kanisa la "Gospel Fire Cathedral", lenye madirisha ya vioo na dari ya mbao, linahusika tu na mambo ya kiroho, si ya kisiasa. Anasema " Sisi sio wafuasi wa kisiasa."

Nguvu za vyama vya siasa katika maeneo ya Zimbabwe.

Muungano wa wa kuhimiza mabadiliko ya kwa raia wa Zimbabwe wa Chamisa (CCC) kwa kawaida una nguvu zaidi katika maeneo ya mijini, lakini Mbare kwa hali ni tofauti kwa upande huo chama cha  ZANU-PF kimekuwa na ushawishi.

Takwimu za serikali ya Zimbabwe zinaonesha zaidi ya asilimia 40 ya watu wanaishi katika umasikini uliokithiri na upatikanaji wa ajira pia ni changamoto kubwa. Lakini katika eneo hilo ambalo kijadi lina ushawishi wa ZANU-PF muumini Anna Mukudo anasema "Tunahitaji ajira zaidi." Anasema ana matumanini uchaguzi ujao wa Agosti 23 utaleta mabadiliko na maboresho.

Soma zaidi:Zimbabwe yashutumiwa kukiuka taratibu kabla ya uchaguzi

Hata hivyo anasema hajui nani atashinda katika uchaguzi huo, lakini Mungu ndiye mjuzi wa hilo.

Chanzo: AFP