1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri aliyetekwa na waandishi wa habari aokolewa

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CguC

COLOMBO.Kikosi cha makomando wa Sir Lanka kimevamia kituo cha televisheni ya nchi hiyo na kumuokoa Waziri wa kazi aliyekuwa akishikiliwa mateka na waandishi wa kituo hicho.

Waziri huyo Meryn Silva alikwenda katika kituo hicho na kumtukana mkurugenzi wa kituo hicho kwa kile alichodai kushindwa kuirusha hewani hotuba yake aliyoitoa wakati wa sherehe za ufunguzi wa daraja.

Daraja hilo ni miongoni mwa yale yaliyoharibiwa na tsunami mnamo mwaka 2004.

Picha za televisheni zilimuonensha waziri huyo akiwa kashikiliwa katika chumba kidogo na wafanyakazi wa kituo hicho wakimtaka kumuomba radhi mkurugenzi wao.