1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu aidhinisha makubaliano ya Kyoto.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW48

Sydney. Waziri mkuu wa Australia Kevin Ruud ameidhinisha makubaliano ya Kyoto ya mabadiliko ya hali ya hewa katika hatua ya kwanza rasmi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo. Hatua hiyo inamaliza upinzani wa muda mrefu wa Australia dhidi ya makubaliano hayo ya Kyoto.

Rudd na baraza lake la mawaziri waliapishwa leo Jumatatu, siku tisa baada ya kushinda katika uchaguzi ambao umemaliza miaka 11 ya utawala wa kihafidhina chini ya John Howard.

Rudd ameweka suala la mapambano dhidi ya ongezeko la ujoto duniani juu katika ajenda, likitiwa nguvu na uuzaji nje wa maliasili. Pia ametangaza mipango ya kuyaondoa majeshi ya Australia yaliyobaki kutoka Iraq.