1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu aliyetimuliwa madarakani Thaksin arudi Nyumbani

28 Februari 2008

Thaksin Shinawatra apokelewa na mamia ya wafuasi

https://p.dw.com/p/DEdz

BANGKOK

Waziri mkuu wa Thailand aliyetimuliwa madarakani Thaksin Shinawatra amewasili nyumbani baada ya miezi 17 ya kuishi uhamishoni.Mamia ya wafuasi wake wamemiminika katika uwanja wa ndege wa Bangkok kumpokea kiongozi huyo. Awali akizungumza na waandishi wa habari akiwa mjini HongKong Thaksin alisema hana mpango wa kurudi katika siasa lakini amefahamisha kwamba yuko tayari kujisalimisha kwenye mikono ya polisi kabla ya kwenda mahakama kuu kuomba dhamana juu ya mashataka ya rushwa dhidi yake. Ameongeza kusema anahakika kwamba mahakama ya Thailand itamkuta bila hatia. Jeshi lilimpindua madarakani Thaksin katika mapinduzi yasiyokuwa na umwagikaji damu mwaka 2006 kwa madai kwamba anahusika katika ulaji ruhswa pamoja na utumiaji mbaya wa madaraka.Hali ya usalama imeimarishwa mjini Bangkok kabla ya kuwasili kwake.