1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa India yuko safarini Beijing

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coxt

BEIJING:

Waziri mkuu wa India-Manmohan Singh yuko Beijing China kwa ziara rasmi ya siku tatu.Lengo la zira yake ni kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.Be Singh alipangiwa kukutana kwa mazungumzo na rais wa china-Hu Jintao pamoja na Waziri mkuu mwenza Wen Jiabao.Ziara yake ndio ya kwanza kufanywa na Waziri mkuu wa India kwa kipindi cha miaka mitano iliopita, na imekuja wakati nchi hizo mbili zikiwa zina uhusiano mzuri wa kibiashara.Hata hivyo uhusiano wa kisiasa umekuwa unatatizwa na kutoamiana kuhusu suala la mpaka ambalo halijapatiwa ufumbzi.Mvutano wa kimpaka ulipelkea nchi hizo kupigana kwa mda mfupi mwaka wa 1962.