1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Italy ajiuzulu

Siraj Kalyango25 Januari 2008

Je! ni uchguzi mypa ama kuteuliwa kwa serikali ya mpito

https://p.dw.com/p/CxWT
Bw Romano Prodi aliejiuzulu kama waziri Mkuu wa Italy baada ya kushindwa katika kura ya kutokuwa na maoni iliopigwa na baraza la Senate.Picha: AP

Waziri Mkuu wa Italia –Ramano Prodi amejiuzulu baada ya ya kipindi kigumu kufuatia kujiuzulu kwa kushindwa katika kura ya kutokuwa na imani nae iliopigwa na baraza la senate.

Hatimae baada ya kipindi kigumu cha miezi 20 Prodi,ambae alipewa jina la kupanga la ‘Il Professore’ kwa maana ya Professor ameachia ngazi rasmi hiyo jana. Hata hivyo ataendelea kuongoza wakati wa mpito hadi kufanyika uchaguzi kabla ya wakati.

Bw Prodi ni mwana uchumi na alitoa hutuba kali katika baraza la Senate kabla ya kujiuzulu kufuatia kuporomoka kwa serikali yake kuliko sababishwa na kujiondoa kwa mjumbe wa serikali yake ya mrengo wa kati- kushoto, hapo kabla.Katika hotuba hiyo Prodi alitetea serikali yake na kuomba kuungwa mkono katika kura ya maoni ya kutokuwa na imani nae.

Hata hivyo alishindwa katika baraza la senate na kura tano. Alipata kura 156 na wapinzani kupata kura 161 hivyo akaiuzulu.

Lakini rais- Giorgio Napolitano- amemuomba Prodi kuendelea kushikilia ofisi hadi utakapo fanyika uchaguzi.

Prodi mwenye Umri wa miaka 68,licha ya kuondokewa na ushirika wa chama cha mrengo wa kati cha kikatoliki cha UDEUR,mapema wiki hii, aliamua kujaribu bahati yake kukabiliana kwanza na baraza la senate licha ya kuombwa na viongozi kadhaa wa kisiasa,akiwemo Napolitano,kujiuzulu.

Kabla ya kupigwa kura,kulitokea sakata ndani ya baraza la Senate.Mjumbe mmoja wa chama cha UDEUR alitangaza kuwa amebadili amebadili msimamo wake na kuwa angempigia kura Prodi.Hilo lilipelekea mkuu wa wabunge wa chama hicho katika baraza hilo kumtupia maneno makali kwa mbunge huyo.Mbunge huyo alievurumishiwa matusi,hakujizuia bali kulia na baadae alibebwa kwa machela kupelekwa nje ya kikao.

Hatua ya kujiuzulu inaleta ombwe la uongozi nchini humo.Kikatiba hali kama hiyo ikitkea ,rais wa nchi hiyokufuatia uashauri na viongozi wa vyama pamoja na wabunge zote mbili,aidha anaweza kuitisha uchaguzi ama kuunda serikai ya mda.

Na sasa rais anafanya mashauriano na viongozi wa kisiasa kuona ikiwa kuna uwezekano wa kuepuka uchaguzi wa mapema kufuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu prodi bada ya kura ya kutokuwa na imani nae.

Rais Napolitano angependelea serikali ya mda ili kufanya mageuzi ya uchaguziu yanayohitajika sana.Lakini upinzani wa mrengo wa kulia unataka uchaguzi mpya. Walitoa mwito huo tangu kashese ianze iliopelekea waziri wa sheria wa serikali ya Prodi kujiuzulu.

Mtangulizi wa Prodi,Silvio Berlusconi, anahamu sana ya kurejea madarakani baada ya kuwa upandewa upinzani kwa kipindi cha miezi 20.

Berlusconi na kiongozi wa ushirika wa kitaifa-Gianfranco Fina,mara tu baada ya habari za Bw Prodi kujiuzulu kutolewa mara moja waliitoa mwito w kufanyika tena uchaguzi mpya.lakini yeye Meya wa jiji la Roma Walter Veltron amehimiza kufanyiwa kwa mageuzi katika mfumo wa uchaguzi, akitoa hoja kuwa uchaguzi mpya chini ya mfumo uliopo utaidumbukiza nchi hiyo katika kile alichoita hali mbaya.

Berlusconi, mwenye umri wa miaka 71, na tajiri anaemiliki vyombo kadhaa bya habari,hajakubali moyoni na hali iliopelekea kushindwa na Prodi na kura elf 24 tu katika uchaguzi uliokuwa mkali wa mwezi Aprili mwaka 2006.

Sasa ikiwa kutafanyika uchaguzi mypa ama kupatika kwa serikali ya mito,kutategemea matokeo ya mkutano unaondelea kwa sasa kati ya rais wa nchi na viongozi mbalimbali wa kisisa nchini humo.