1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Lebanon atangaza siku moja ya maombolezi

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyjZ

BEIRUT:

Waziri Mkuu wa Lebanon-Faoud Sinora,ametangaza siku ya maombolezo-siku moja tu baada ya watu saba kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maandamano ya ghasia katika mji mkuu wa Beirut.Maafisa wanasema kuwa, waandamanaji ambao walikusanyika kuandamana kupinga kukatwa umeme kwa kila mara ,walichoma matairi na kuzuia barabara.Jeshi lilifyatua risasi lilipoingilia kati kuweza kufungua barabara zilizokuwa zimewekewa vizuizi.