1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Serbia atoa wito wa mazungumzo zaidi kuhusu Kosovo.

9 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZGo

Belgrade. Waziri mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica ametoa wito wa kuwa na mazungumzo zaidi kuhusu hali ya baadaye ya jimbo la Serbia la Kosovo. Katika taarifa Kostunica amesema majadiliano ndio njia pekee ya kuepusha mzozo mkubwa zaidi. Urusi tayari imekwisha sema inaunga mkono kuendelea kwa mazungumzo, lakini Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Itali zimesema zinapinga hatua hiyo. Katika taarifa ya pamoja mataifa hayo manne yamesema kuwa kile kinachoitwa kundi la pande tatu la wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya , Marekani na Russia wamefikia mwisho wa juhudi zao za kutatua mzozo huo. Kuna aina fulani ya ukweli, na ukweli huo ni kwamba kundi la pande tatu ambalo limefanyakazi kwa nguvu zake zote na nafikiri kwakweli limepiga hatua kwa kuzileta pande hizi mbili kuweza kuzungumza kwa mara ya kwanza katika muda mrefu. Nafikiri wameweka misingi muhimu , lakini nahisi kuwa hatua hizi zimefikia mwisho.

Wakosovo wenye asili ya Albania waliowengi katika jimbo hilo hivi sasa wanatarajiwa kutangaza uhuru kutoka Serbia. Waziri mkuu wa Serbia amesema kuwa hatua hiyo itakuwa kinyume na sheria na itakuwa na matokeo yasiyo tarajiwa. Kutokana na uwezekano wa kutokea ghasia kuongezeka , jeshi la NATO limependekeza kuweka wanajeshi wake 17,000 wanaolinda amani katika jimbo hilo la Serbia.