1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Ugiriki Samaras kukutana na Kansela Merkel Berlin

24 Agosti 2012

Kabla ya mkutano wake na waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras ,kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo (24.08.2012), maafisa wa serikali mjini Berlin wanajaribu kupooza hamasa za matarajio ya mkutano huo.

https://p.dw.com/p/15vvQ
Antonis Samaras waziri mkuu wa Ugiriki
Antonis Samaras waziri mkuu wa UgirikiPicha: Reuters

Uamuzi wa iwapo Ugiriki ipatiwe fungu jingine la mkopo wake, hautachukuliwa , hadi itakapotolewa ripoti ya wakopeshaji wakuu wa Ugiriki , halmashauri ya Ulaya, benki kuu ya Ulaya na shirika la fedha la kimataifa IMF, mwezi Septemba.

Kila mmoja anafahamu hata hivyo mjini Berlin , kile ambacho spika wa bunge la Ulaya alichosema katika mahojiano. Ni kwamba pande hizo tatu katika ripoti yake haitatoa kwa Ugiriki hukumu ya , "mmefanya vizuri sana", lakini itaitaka nchi hiyo kuongeza juhudi na kupiga hatua zaidi. Lakini ni kwanini basi kabla ya ziara hii ya waziri mkuu wa Ugiriki tayari kumefikiwa uamuzi wa kuitakia kila la kheri Ugiriki kuhusiana na mipango yake ya mageuzi.?

Samaras aonekana kuwa kimya

Merkel anajizuia kumpa ukweli Samaras ambaye ni mhafidhina. Akiwa kama kiongozi wa upande wa upinzani aliongoza mpango wa mageuzi kwa ajili ya Ugiriki. Kansela amekuwa akirudia tena pamoja na viongozi wengine wa kihafidhina wa Ulaya, kuwa anatakiwa aongoze, lakini Samaras amekuwa kimya.

Mara alipochukua wadhifa huo wa waziri mkuu, aliweka kando ahadi zake za wakati wa uchaguzi, na kila kitu kinakwenda sasa katika mipango inayotakiwa tu na kundi hilo la pande tatu, na kwamba ni lazima atekeleze mpango wa kupunguza matumizi unaofikia kiasi cha euro bilioni 11.5.

Je Merkel anaweza kumuamini mtu kama huyu, kwamba atakuwa na uwezo wa kutekeleza mpango wa kubana matumizi na kuendelea na mageuzi?.

Hadi sasa nia ya mageuzi inaonyesha kuwa ni sawa na methali inayosema mtumikie kafiri upate mradi wako.

Mtazamo wa serikali mjini Berlin ni kuwa , tutafanikisha , kile ambacho ni sahihi kwa ajili ya euro, amesema msemaji wa serikali Steffen Seibert akiizungumzia Ugiriki. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema alipokutana na rais wa ufaransa Francois Hollande kuwa Ugiriki inapaswa kuchukua juhudi maalum ili kuweza kubakia katika zoni ya mataifa ya sarafu ya euro.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wajaribu kila njia kuinusuru sarafu ya Euro
Rais wa Ufaransa Francois Hollande na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wajaribu kila njia kuinusuru sarafu ya EuroPicha: picture-alliance/dpa

Kwangu mimi ni muhimu, kwamba kila mmoja wetu awajibike. Na tusubiri ripoti ya kundi la pande tatu, na kuona matokeo yake ni yapi. Lakini tunaitaka Ugiriki, na mimi binafsi naitaka Ugiriki kuongeza juhudi katika mageuzi, ambayo hata watu wa Ugiriki wanayataka.

Si watu wengi wanahofu ya kuporomoka kwa mataifa ya eneo la euro, ambapo mataifa makubwa wanachama wa umoja wa Ulaya yanaweza kutumbukia katika msukosuko mkubwa. Bila shaka katika hali hii mfuko wa uokozi wa umoja huo ESM, utatosha kuzipatia mikopo nchi hizi.Hata hivyo iwapo kutatokea hali ya kuvunjika kwa eneo la euro, mradi wa umoja wa Ulaya kwa hivyo unaweza kuwa mashakani. Ikitokea hali kama hiyo anasema kansela kuwa suala si maslahi ya kiuchumi badala yake ni kuimarisha ushirikiano wa kisiasa kwa ajili ya bara lote la Ulaya.

Mwandishi: Kouparanis, Panagiotis/ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo