1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Rice kukutana na Rais Abbas

P.Martin5 Novemba 2007

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice hii leo atakutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas.

https://p.dw.com/p/C77G

Siku ya Jumapili,Rice alikuwa na majadiliano pamoja na viongozi wa Kiisraeli katika jitahada ya kuendeleza mpango wa kuunda taifa la Palestina.Amesema,

„Machafuko ya itikadi kali kimsingi yamezindua mkakati wa mfungamano mpya katika Mashariki ya Kati.Mataifa yenye kuwajibika ambayo hapo awali yalikuwa mahasimu,sasa yameona kuwa maslahi yao labda ni moja-kupambana na kitisho cha aina moja.Pia taifa la Palestina lenye siasa za wastani ni kinga dhidi ya kitisho hicho.“

Kwa upande mwingine Waziri wa Nje wa Israel,Tzipi Livni amemuambia waziri mwenzake Rice kuwa Israel haitotekeleza mpango wo wote utakaopendekezwa na Marekani,kabla ya kuhakikishiwa usalama wake.