1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Tanzania atenguliwa kwa ukatili dhidi ya mfanyakazi

Deo Kaji Makomba
27 Novemba 2023

Jeshi la polisi nchini Tanzania limemhoji aliekuwa naibu waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul kwa tuhuma za kumfaynika ukatili mfanyakazi ambaye amedai aliingizwa chupa kwenye sehemu za siri akidaiwa kutaka kumuua.

https://p.dw.com/p/4ZUjw
Tanzania|Naibu waziri wa zamani wa Katiba an Sheria  Pauline Gekul
Aliekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul anadaiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake akidai kuwa alikuja hotelini kwake kimkakati.Picha: Ericky Boniphace/DW

Wakati polisi ikimhoji Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul kufuatia tuhuma za ukatili na unyanyasaji dhidi ya mfanyakazi wake Hashim Ally, wanasheria na wanaharakati wa haki za binadamu wametoka hadharani na kutaka hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya mbunge huyo endapo tuhuma zinazomkabili zitathibitika kuwa za kweli.

Mbunge Gekuli anatuhumiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana wake kumwingizia chupa sehemu ya siri ya haja kubwa mfanyakazi wake, Hashimu Ally au kumpiga risasi kwa madai ya kwamba alitumwa kimkakati kwenda kwenye hoteli yake ya Paleii Lake View Garden.

Sakata hilo liliibuka baada ya video kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Tanzania, ikimuonyesha Hashimu akieleza jinsi alivyofanyiwa ukatili huo na Gekuli ambaye hadi majuzi alikuwa ni Naibu Waziri wa katiba na Sheria kabla ya kutumbuliwa na Rais Samia Suluhu HassanJumamosi usiku ingawa sababu za kutumbuliwa kwake hazikuwekwa bayana.

Tazania| Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia Suluhu Hassan alitengua uteuzi wa Gekul Jumamosi usiku pasina kutoa sababu ya uamuzi huo, kabla habari zake kuenea kuhusu ukatili aliomfanyia mfanyakazi wake.Picha: Ericky Boniphace/AP/picture alliance

Akizungumza na DW, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binada nchini Tanzania, LHRC, Anna Henga, amesema kitendo alichotendewa kijana huyo cha kuingiziwa chupa katika sehemu ya siri ya haja kubwa ni kitendo cha kinyama na kwamba kama itathibitika ni kweli mbunge huyo alishiriki kwa namna moja ama nyingine, basi hatua za kisheria zinapaswa kuchukuliwa ili kuleta usawa kwa jamii.

Soma pia: Polisi ya Arusha ilimshilikilia Lissu pamoja na wenzake watatu kwa mahojiano kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isivyo halali

"Tukiipa nafasi mahakama ikachukuwa ushahidi vizuri ikaweza kuhukumu kwa haki, kwa sababu kitendo alichofanyiwa huyo kijana ni kibaya sana kama itathibitika ni kweli," alisema Henga.

Polisi yasema inaendelea kuchunguza

Tukio hilo la kijana Hashim Ally kufanyiwa kitendo cha ukatili na unyanyasaji limepokelewa kwa kwa maoni mseto na wananchi wa kawaida huku nao wakitaka sheria zichukuliwe endapo itabainika mbunge huyo alishiriki katika unyama huo kwa namna moja ama nyingingine.

"Mimi nadhani sehria ifuate mkondo wake, uchunguzi ufanyike, na iwe fundisho kwa watu wanaotumia vibaya madaraka yao au nyadhifa waliozopewa na serikali ili kuwakomesha watu wasiokuwa na uwezo," alisema George Kasela, mkaazi wa jijini Mwanza.

Tanzania | Inspekta Jenerali mkuu wa Polisi Camillius Wambura
Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania, IGP, Camillius WamburaPicha: Ericky Boniphace/DW

Kufuatia taarifa hizo kusamabaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku wana harakati wa masuala ya haki za binadamu nchini Tanzania wakipaza kelele kuhusiana na kitendo hicho cha kinyama  alichofanyiwa kaijana Hashim Ally, jeshi la polisi mkoani Manya lilithibitisha kumkamata Mbunge Gekul jana Jumapili na kumfanyia mahojiano.

Soma pia:Rais wa Tanzania awaapisha viongozi walioteuliwa hivi karibuni 

Kamanda wa polisi mkoani Manyara George Katabazi alithibitisha kukamatwa kwa mbunge Pauline Gekul na kwamba wanaendelea na uchukuzi wa tukio hilo.

Pauline Gekul amabye alikuwa ni Naibu Waziri wa katiba na sheria nchini Tanzania, uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Juzi Jumamosi usiku huku sababu za kuondolewa katika wadhifa huo hazikuwekwa bayana, lakini watu mbalimbali wakihusisha kutenguliwa huko kunatokana na tuhuma zinazomkabili mbunge huyo.