1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lauterbach alenga kuhalalisha matumizi ya bangi

20 Januari 2024

Waziri wa afya wa Ujerumani Karl Lauterbach anashikilia msimamo wake wa kutaka kuhalalisha matumizi ya bangi kwa kuwasilisha muswada mbele ya bunge mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/4bV6j
Uvutaji wa bangi
Hapa Ujerumani, watu wazima wataruhusiwa kupanda mimea ya bangi na kumiliki kiasi kidogo cha bangi kuanzia Aprili mosi.Picha: picture-alliance/dpa/Leukert

Hii ni licha ya upinzani ndani ya muungano wa vyama vinavyounda serikali inayoongozwa na Kansela Olaf Scholz.

Lauterbach ameliambia gazeti la Ujerumani la Die Welt kuwa, ana matumaini kuwa muswada wa kuhalalisha matumizi ya bangi utapitishwa na bunge kati ya Februari 19 na 23 na kwamba, utakuwa sheria kuanzia Aprili mosi.

Hata hivyo wabunge ndani ya chama cha Social Democrats, ambapo Lauterbach na Scholz ni wanachama, wameonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo.

Muungano huo tawala, unaojumuisha chama cha kijani na kile cha waliberali FDP, ulikubali mwishoni mwa mwezi Novemba kuondoa bangi kwenye orodha ya vitu vilivyopigwa marufuku.

Iwapo muswada huo utapitishwa na kuwa sheria, watu wazima wataruhusiwa kupanda mimea ya bangi na kumiliki kiasi kidogo cha bangi kuanzia Aprili mosi.