1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani awakumbuka watu waliokufa kutokana na mafuriko ya Sunami huko Indonesia.

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBI1

Jakarta:

Waziri wa maendeleo ya kiuchumi wa Ujerumani, Bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul, wakati akifanya ziara katika jimbo la Aceh huko Indonesia amewakumbuka watu waliokufa kutokana na janga la mafuriko ya Sunami miaka miwili iliopita. Aliweka shada la mauwa katika kaburi la pamoja karibu na mji mkuu wa jimbo hilo, Bandar Aceh. Katika jimbo hilo huenda zaidi ya watu 170,000 walikufa kutokana na mafuriko hayo ya bahari. Bibi Wieczorek-Zeul aliahidi kwamba Ujerumani itatoa Euro nyingine milioni 20 kusaidia katika ujenzi mpya wa jimbo hilo.