1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani azuru Iraq huku Uturuki ikituma jeshi lake kuwasaka wapiganaji wa PKK

Siraj Kalyango18 Desemba 2007

Mgogoro kati ya Uturuki na PKK ulianza 1984

https://p.dw.com/p/Cd7e
Mpiganaji wa kundi la waasi wa Wakurdi wa Uturuki-maarufu kama PKK akiwa karibu na mpaka wa Iraq na Uturuki Oktoba 28,2007.Picha: AP

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani-Condoleezza Rice yuko Iraq huku mgogoro kati ya WaKurdi na Uturuki kuingia sura mpya kufuatia hatua ya majeshi Uturuki kuingia katika maeneo hayo.

Ziara ya Bi Condoleezza Rice nchi Iraq haikutangazwa mapema.

Na inaelezwa kuwa nia ya safari hii ni kuunga mkono juhudi za maridhiano za mjumbe mpya wa Umoja wa Matiafa nchini Iraq, Steffan de Mistura, katika eneo lenye tofauti sio tu za kidini lakini pia za kikabila.Eneo hilo ni la Wakurdi.

Bi Rice aliwasili katika mji wa jimbo hilo la kaskazini mwa nchi hiyo wa Kirkuk bila kutangazwa kutokana na sababu za kiusalama.

Akiwa huko atakutana na wajumbe wa jamii za wakurdi,wa arab wa kisunni na kishia,pamoja na jamii za Kikristo na Kiturkimen.

Jumatatu waziri mkuu waserikali ya kijimbo ya Kikurdi- Nechirvan Barzani, alisema kuwa utawala wake unaunga mkono kucheleweshwa kwa mda wa miezi sita wa kura ya maoni kuhusu siku za baadae za Kirkuk.

Tamko hilo limepunguza wasiwasi miongoni mwa wananchi waliogawanyika.Kifungu namba 140 cha katiba ya Iraq kinasema kuwa kura ya maoni inapashwa kufanywa ifikapo mwisho wa mwaka wa 2007 ili kuamua ikiwa jimbo hilo lenye utajiri wa mafuta,liwe chini ya utawala wa serikali huru ya waKurdi.

Ziara ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani nchini Iraq, imekuja wakati ikiarifiwa kuwa wanajeshi karibu 300 wa Uturuki wakiwa wameingia katika ardhi ya Iarq kwa lengo la kuwasaka wapiganaji wa Kikurdi wanaoshambulia wakitokea katika maeneo hayo.hat hivyo serikali ya Ankara haijatoa taarifa yoyote kuhusu jambo hilo.

Msemaji wa kikosi cha usalama cha Wakurdi wa Iraq cha Peshmerga-Jabbar Yawara ameliambia shirika la habari la kifaransia la AFP kuwa wanajeshi wa Uturuki waliaingia kaskazini mwa Iraq asubuhi ya leo.

Hii ndio operesheni ya kwanza kwa vikosi vya Uturuki kupenya katika ardhi ya Iraq, tangu kuwepo mvutano kati ya utawala wa Ankara Baghdad kuanza mwezi Oktoba kuhusu waasi wa Kikurdi.

Jabar Yawar amenukuliwa akisema kuwa eneo ambalo jeshi la uturiki limeingilia ni jangwa ambako hakuna kikosi chochoite cha Iraq wala cha Peshmerga.

Kituo kimoja cha televisheni cha Kikurdi chenye kumilikiwa na chama cha tawala huko cha Massud Barzani kimesema kuwa wanajeshi wa Uturuki wameingia kilomita kadhaa ndani mwa Iraq.

Mvutano kati ya Uturuki na Iraq ulianza Oktoba 21 wakati waasi wa kikurdi wa PKK waliposhambulia askari wa uturuki na kuwauwa 12 kati yao. Tangu wakati huo Uturuki imekuwa inatishia kuanza mashambulizi ya kijeshi nchini Iraq kuwasaka wapiganaji hao.

Bunge la Uturuki nalo litoa ruhsa kwa vikosi vyake kufanya mashambulizi hayo.

Kundi la PKK limekuwa likipigania eneo lao la kusini mwa uturuki kujitawala tangu mwaka wa 1984,na watu zaidi ya laki 3 wamepoteza maisha yao katika mgogoro huo kwa pande zote mbili.

Serikali ya kijimbo ya Wakurdi wa Iraq imelaani kujipenyeza huko kwa jeshi la Uturuki.