1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani ziarani Aceh

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiv

Banda Aceh:

Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Heidemarie-Wieczoreck-Zeul analitembelea jimbo la Aceh nchini Indonesia,miaka miwili baada ya janga la Tsunami kupiga katika eneo hilo.Mkurugenzi wa idara ya ujenzi mpya,Kuntoro MANGKUSUBROTO,amemuelezea jinsi shughuli za ujenzi mpya,zinazogharimiwa zaidi kwa msaada wa maendeleo wa Ujerumani zinavyoendelea.Hii leo waziri Heidemarie Wieczoreck-Zeul analitembelea kwa helikopta eneo hilo la maafa.Watumishi kadhaa wa mashirika ya misaada ya maendeleo ya ujerumani wanasaidia katika jimbo la Aceh,ikiwa ni pamoja na watumishi wa shirika la misaada ya kiufundi na jumuia ya ushirikiano wa kiufundi GTZ.