1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani ziarani Angola

4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWfv

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Michael Glos akiwa ziarani nchini Angola amesifu maendeleo ya kiuchumi yaliyopatikana katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.Amesema,Angola baada ya kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa sasa imenyanyuka kiuchumi na inaweza kulipa deni lake la Dola bilioni 1,8 kwa kundi la wafadhili linalojulikana kama Klabu ya Paris.Deni hilo litalipwa kwa awamu tatu.