1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi na mshauri wake watimuliwa Nigeria

23 Juni 2012

Rais Goodluck Jonatahan wa Nigeria, amemfukuza kazi Waziri wa ulinzi pamoja na mshauri wake, hku kukiwana ongezeko jipya la mashambulizi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali la Boko Haramu.

https://p.dw.com/p/15KAj
©Jonathan Rebboah/Wostok Press/Maxppp France, Paris 25/11/2011 Le president du Nigeria Goodluck Jonathan arrive au palais de l Elysee The President of Nigeria Goodluck Jonathan at the Elysee Palace
Goodluck JonathanPicha: picture alliance / dpa

Taarifa za kufukuzwa kazi Waziri Bello Mohammed na mshauri wake Andrew Owoye Azazi zimetolewa na msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo Reuben Abati na kuchapishwa kwenye gazeti moja maarufu la kila siku nchini humo.

Nafasi ya Azazi imechukuliwa na Kanali mstaafu Sambo Dasuki kiongozi maarufu kutoka eneo la kaskazini na binamu wa Sultani wa himaya ya Sokoto.

Dasuki alihusishwa pia katika jaribio la kufanya mapinduzi mwaka 1995 dhidi ya utawala wa kidikteta wa Rais wa zamani San Abacha, na kukimbilia uhamishoni nchini Marekani. Hadi sasa hakuna taarifa kamili kuhusu mtu atakayechukua nafasi hiyo ya uwaziri wa ulinzi.

Uamuzi baada ya kurejea kutoka Rio

Rais Jonathan amechukua hatua hiyo mara baada ya kurejea kwenye mkutano wa mazingira duniani uliofanyika mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil. Uamuzi wa rais huyo kuhudhuria mkutano huo kimekosolewa vikali na watu mbalimbali nchini mwake, baada ya Boko Haramu kufanya mashambulizi kwenye makanisa Jumapili iliyopita mjini Kaduna.

Mashambulizi hayo yaliyozusha hasira miongoni mwa wakristo na kusababisha vurugu ambapo watu 110 waliuawa. Rais Jonathan aliondoka nchini humo siku ya Jumanne kwenda Brazil, licha ya kuwepo kwa mashambulizi hayo mapya.

Kituo cha polisi Nigeria
Kituo cha polisi NigeriaPicha: Reuters

Nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta, imegawika katika sehemu mbili ya kaskazini ambayo inakaliwa na waislamu na kusini inayokaliwa na wakristo.

Mshauri Azazi ni mshirika wa kisiasa wa Rais Jonathan amabye wanatokea sehemu moja jimbo la Balyesa lenye utajiri wa mafuta kusini mwa nchi hiyo. Azazi anashukuiwa na watu wa eneo la kaskazini kuhusika na machafuko hayo, kufuatia kauli yake aliyoitoa mwezi Aprili inayoonyesha kuwa matukio hayo yana msukumo wa kisiasa.

Wananchi waendelea kuilaumu serikali

Hali ya uvunjifu wa amani kwenye baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ilianza Jumapili iliyopita kwenye jimbo la Kaduna baada ya makanisa matatu kulipuriwa kwa mabomu ya kujitoa mhanga na kuwauwa watu 16. Tukio hilo lilizusha hasira miongoni mwa wakristo ambao nao walianza kuchoma moto misikiti na kuuwa waislamu wengi.

Vurugu zaidi ziliibuka jimboni Kaduna wiki hii ambapo siku ya Jumatatu na Jumanne mapambano baina ya polisi na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la Boko Haramu kwenye mji wa kaskazini wa Damaturu yaliwaacha watu 40 wamekufa.

Moja ya miripuko nchini Nigeria
Moja ya miripuko nchini NigeriaPicha: picture-alliance/dpa

Raia nchini humo wamezidi kuikosoa serikali kwa namna inavyoishughulikia hali hiyo kutokana na washambuliaji kutumia silaha nzito huku utawala ukwa haueleweki unafanya mbinu gani kukomesha mauwaji ya watu.

Mwandishi: Stumai George/AFP/ DPA

Mhariri: Sekione Kitojo