1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi Ujerumani aanza ziara, Mataifa ya Baltic

25 Septemba 2023

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amewasili Jumatatu katika mji mkuu wa Latvia, Riga - akianza ziara ya siku tatu katika Mataifa ya Baltic.

https://p.dw.com/p/4Wmtz
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alipotua katika uwanja wa ndege wa Riga, mji mkuu wa Latvia.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alipotua katika uwanja wa ndege wa Riga, mji mkuu wa Latvia.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture-alliance

Pistorius akiambatana na ujumbe wake, anatarajia kufanya mazungumzo kuhusu hali jumla ya usalama na ushirikiano zaidi wa kijeshi na Latvia ambayo pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO.

Kesho Jumanne, Ujumbe wa Ujerumani utaelekea Estonia kunakotarajiwa Mkutano wa kila mwaka wa ulinzi wa kanda hiyo ya Baltic. Ujerumani imezidisha kwa kiasi kikubwa ushiriki wake wa kijeshi katika Mataifa ya Baltic baada ya Urusi kuanzisha vita vyake dhidi ya Ukraine.

Berlin imekua ikishirikiana mno na Lithuania na inapanga katika siku za usoni kutuma nchini humo kikosi kitakachokuwa tayari kwa mapambano.

Ujerumani yakaribia kufanya maamuzi ya kupeleka makombora ya kisasa kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi