1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani imeamuaje juu ya vifaru vya kivita?

Bruce Amani
24 Januari 2023

Waziri mpya wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amesema kuwa anatarajia uamuzi wa haraka juu ya upelekaji wa vifaru vya kivita aina ya Leopard nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4Mdjs
Deutschland Bundeswehr Kampfpanzer Leopard 2 A7V
Picha: Philipp Schulze/dpa/picture-alliance

Akizungumza mjini Berlin katika mkutano na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, Pistorius amesema masuala ya kama vile ya matengenezo, ukarabati na upelekaji upya wa zana za kivita yanachunguzwa kabla ya kupelekewa vifaru hivyo.

Pistorius amezihimiza nchi washirika ambazo zina vifaru chapaLeopard vinavyofanya kazi tayari kuanza kuwapa mafunzo wanajeshi wa Ukraine ya jinsi ya kuvitumia.