1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Itachukua miezi kadhaa kushinda vita Ukanda wa Gaza

Tatu Karema
14 Desemba 2023

Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant, leo amemwambia mshauri wa usalama wa kitaifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan kwamba itachukua miezi kadhaa kushinda vita dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

https://p.dw.com/p/4aARV
Ukanda wa Gaza- Israel | Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Marekani Jake Sullivan na Waziri wa Ulinzi Israel Yoav Gallant.
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Marekani Jake Sullivan akizungumza na Waziri wa Ulinzi Israel Yoav Gallant. Picha: ISRAELI GOVERNMENT PRESS OFFICE (GPO)/Anadolu/picture alliance

Gallant amesema kwa zaidi ya muongo mmoja , kundi hilo limekuwa likijenga miundo mbinu ya chini na juu ya ardhi na kwamba kuliangamiza kundi hilo kutahitaji muda wa miezi kadhaa. Hata hivyo Gallant amemuhakikishia Sullivan kwamba watashinda vita hivyo.

Taarifa kutoka afisi ya Gallant, imesema kuwa wawili hao pia wamezungumzia haja ya Waisraeli kurejea katika makazi yaokaribu na mpaka wa Lebanon baada ya maelfu ya watu kupoteza makazi yao kutokana na mapigano na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran. 

Soma pia:Raia wengi wa Gaza wanakimbilia eneo la mpakani na Misri wakihofia mapigano kati ya Israel na Hamas

Haya yanajiri wakati jeshi la Israel limetangaza kusitisha mapigano kwa masaa manne katika kitongoji cha al-Salam cha Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza kuwaruhusu raia kupata mahitaji zaidi muhimu kama vile chakula na maji.