1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAZIRSTAN:Wataleban zaidi wauawa

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBg3

Majeshi ya Pakistan yamewaua wanamgambo sita wa kitaliban katika mapigano yaliyotokea huko Waziristan kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Eneo hilo la Waziristan ambalo liko mpakani na Afghanstan limekuwa katika vurugu kubwa ambapo wapiganaji wa Kitaliban wamejihifadhi wakiungwa mkono na wenyeji wa eneo hilo waliyokataa mpango wa amani na serikali wiki iliyopita.

Serikali ya Pakistan imesema kuwa imeanzisha harakati kubwa dhidi ya wanamgambo wa kitaliban katika eneo hilo.