1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wengi wa Arsenal wako nje

6 Novemba 2015

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na orodha inayoendelea kuwa ndefu ya majeruhi katika timu yake. Kuna wachezaji kadhaa ambao wako mkekani

https://p.dw.com/p/1H1Mq
Arsene Wenger beim Arsenal Spiel gegen Norwich
Picha: picture-alliance/AP

Wenger amethibitisha kuwa Hector Bellerin atakosa mchuano wa kesho wa debi ya kaskazini mwa London dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati Laurent Koscielny akitiliwa mashaka ikiwa atakuwa amepona kabisa.

Arsenal wana wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza ambao wako mkekani, wakiwemo beki wa kulia Bellerin na beki wa katikati Koscielny. Alex Oxlade Chamberlain, Theo Walcott na Aaron Ramsy wote wako nje hadi baada ya kipindi cha michuano ya kimataifa wakati Jack Wilshere anatarajiwa kurejea katikati ya Desemba. Toma Rosciky na Danny Welbeck wanatarajiwa kurejea uwanjani Januari mwakani.

Mapungufu hayo yalionekana wakati Arsenal walizabwa magoli matano kwa moja na Bayern katika Champions League katikati mwa wiki, na Wenger anasema sasa ni wakati wa kujinyanyua tena

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: