1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wenger kuondoka Arsenal mwisho wa msimu

Lilian Mtono20 Aprili 2018

Hatimaye meneja wa muda mrefu wa timu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya kandanda ya England, Arsene Wenger ametangaza atanga'atuka kwenye nafasi hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuifundisha timu hiyo kwa miaka 22.

https://p.dw.com/p/2wPj9

Wenger mwenye miaka 68 ameshinda mataji matatu ya Premier akiwa na Arsenal, na kuweka rekodi ya kuwa kocha pekee nchini England kutoshindwa mchezo hata mmoja katika msimu mzima wa 2003-04. Ameshinda pia makombe saba ya FA na kuiwezesha timu hiyo kushiriki michuano ya mabingwa Ulaya kwa miaka 20. Lilian Mtono amezungumza na mchambuzi wa michezo aliyeko Dar es Salaam Tanzania, Master Tindwa, ambaye kwanza ametoa maoni yake kuhusu hatua hiyo ya Wenger.