1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoIvory Coast

Wenyeji wa AFCON Ivory Coast wapangwa kundi moja na Nigeria

Josephat Charo
13 Oktoba 2023

Guinea ya Ikweta na Guinea-Bissau, ambazo zimefuzu kwa mara ya nne mfululizo kwa mashindano hayo pia zimepangwa katika kundi hilo.

https://p.dw.com/p/4XVkG
Elfenbeinküste, Abidjan | Auslosung der Spiele der AFCON-Gruppenphase
Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Wenyeji Ivory Coast imepangwa na Nigeria katika kundi A kwenye mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwakani kufutia droo iliyofanyika jana Alhamisi.

Guinea ya Ikweta na Guinea-Bissau, ambazo zimefuzu kwa mara ya nne mfululizo kwa mashindano hayo pia zimepangwa katika kundi hilo.

Mabingwa watetezi Senegal wako katika C pamoja na washindi mara tano wa kombe la mataifa ya Afrika, Cameroon, pamoja na Guinea na Gambia.

Morocco wamepangwa katika kundi F na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia na Tanzania. Ivory Coast inayaandaa mashindano hayo kwa mara ya pili na inatumai kupata matokeo mazuri kuliko 1984.