1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Westerwelle azuru Misri

Sekione Kitojo19 Aprili 2011

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ameihakikishia Misri kupatiwa misaada ya kiuchumi, lakini pia ameitaka nchi hiyo kusisitiza msimamo wake kuhusu demokrasia.

https://p.dw.com/p/10wbj
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle .Picha: picture-alliance/dpa

Katika ziara yake leo Jumanne nchini Misri waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle , ameihakikishia nchi hiyo msaada wa kiuchumi, lakini kabla ya hapo alitaka nchi hiyo ionyeshe mpango wake kuelekea demokrasia. Taifa linalofuata sheria ni sharti la mwanzo kwa uwekezaji wa makampuni ya Ujerumani nchini humo.

Mkutano na waandishi wa habari katika wizara ya mambo ya kigeni ya Misri- ambapo katika ukumbi huu aliwahi kusimama waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle mwishoni mwa mwezi Februari. Hata hivyo akiwa na viongozi wengine kabisa waliokuwa madarakani. Ahmad Abul Gheit, ambaye hivi sasa ameondolewa. Katika nafasi yake hivi sasa yuko Nabil-al-Arabi, mtu anayechukua tahadhari sana katika utendaji wake na ambaye anamzidi waziri Westerwelle kwa takriban miaka 20.

Nafarijika sana kwamba Bwana Westerwelle amenialika kufanya ziara nchini Ujerumani. Miaka 40 iliyopita niliwahi kuwa balozi nchini Ujerumani na nimejaribu kujifunza Kijerumani amesema Al-Arabi.

Katika mkutano wao wa dakika 40 mawaziri hao wawili wa mambo ya kigeni walijaribu kuzungumzia kuhusu hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati pamoja na hali nchini Libya, pamoja na hususan kuhusu maendeleo nchini Misri. Guido Westerwelle amesema , Al-Arabi amemhakikishia, kwamba Misri itaendelea kubaki katika mpango wake wa kuleta demokrasia nchini humo.

Demokrasia na serikali inayofuata sheria ni vitu vinavyokwenda pamoja. Uchaguzi pamoja na uhuru wa kutoa mawazo vinakwenda pamoja. Makampuni ya Ujerumani ambayo nayahimiza hivi sasa kuwekeza nchini Misri , yanapaswa kufahamu, ni katika nchi ya aina gani yanawekeza, kwa mfano katika msimamo wa kisiasa. Na ndio sababu maendeleo sahihi ya kiuchumi na msisitizo wa kuendelea na mwelekeo wa kidemokrasia ni vitu ambavyo haviwezi kutenganishwa.

Ushirikiano wa kiuchumi , amedokeza mwakilishi mmoja wa vyombo vya habari nchini Ujerumani , ni lazima uende pamoja na sheria za kupambana na rushwa. Na hili alilijibu Nabil al-Arabi, kuwa serikali yake inatekeleza mikataba yote ya kimataifa.

Misri inachukua juhudi zote hivi sasa , kujenga nchi inayofuata sheria. Rushwa zinazofanywa na wanasiasa na katika nyanja za kiuchumi zitafikishwa mbele ya sheria. Ukweli ni kwamba katika siku za hivi karibuni vigogo wa kisiasa wameshtakiwa, ikiwa ni ushahidi , kwamba taifa hili linaheshimu sheria.

Wahlen in Ägypten Hosni Mubarak
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak ambaye alihojiwa hivi karibuni na vyombo vya sheria.Picha: AP

Guido Westerwelle amejiweka katika upande zaidi wa viongozi wenzake wa serikali ya Misri.

Hii , ndio sababu kile uongozi mpya wa Misri unachopambana nacho kuhusu rushwa na pia kujitoa kutoka katika hali ya utawala wa zamani, kimetufanya kutambua juhudi zao.

Mawaziri wote wawili wamesisitiza kuwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya serikali mpya ya Misri na Ujerumani unapaswa kuimarishwa zaidi.

Mwandishi : Saoub, Esther / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman