1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Westerwelle ziarani Afrika

Admin.WagnerD29 Aprili 2013

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Guido Westerwelle yuko ziarani barani Afrika. Baada ya kuizuru Ghana mwishoni mwa juma, leo anakwenda Afrika kusini na baadae ataitembelea Msumbiji

https://p.dw.com/p/18Os5
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujwerumani Guido Westerwelle akiwasili Ghana
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujwerumani Guido Westerwelle akiwasili GhanaPicha: picture-alliance/dpa

Mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria, ni kituo cha pili cha zaira ya siku tano ya Waziri Westerwelle barani Afrika ambapo atakutana na Makamu wa rais Kgalema Motlanthe na Waziri wa mambo ya nchi za nje Maite Nkoana Mashabane.

Afrika kusini ina nguvu kubwa kiuchumi barani humo na kitamaduni ni mshirika mkubwa wa Ujerumani. Mwaka jana pekee kiwango cha kibiashara kati ya nchi hizi mbili kwa bidhaa zinazoagizwa na zinazosafirisha kwenda na kutoka upande mwengine,kilifikia jumla ya euro bilioni 14.

Sawa kama ilivyo Ujerumani, Afrika kusini paia ni mwanachama wa kundi la nchi 20 za viwanda na zile zinazoinukia haraka kiuchumi. Kutoka Afrika kusini,baadae leo Waziri Wester Welle atakwenda mji mkuu wa Msumbiji Maputo, kituo cha mwisho cha ziara yake hiyo ya siku tano barani Afrika.

Ushirikiano kiuchumi

Shirika la Ushirikiano wa kiufundi la Ujerumani GIZ lina wafanyakazi wapatao 250 wa kitaifa na kimataifa nchini Msumbiji wakiwemo karibu 330 waliopelekwa kama wataalamu nchini humo.

Waziri Westerwelle leo (29.04.2013) anazuru Afrika Kusini na Msumbiji
Waziri Westerwelle leo (29.04.2013) anazuru Afrika Kusini na MsumbijiPicha: picture-alliance/dpa

Msumbiji imepata ukuaji uchumi wa mwaka wa karibu asilimia 7 tangu 2006. Lakini pamoja na ukuaji huo wa kiuchumi asilimia 70 ya wakaazi wa nchi hiyo bado wanaishi katika hali ya umasikini. Karibu nusu ya bajeti ya taifa hilo inatokana na msaada wa Wafadhili ikiwemo Ujerumani.

Mchango wa kijeshi kwa Mali

Ziara Westewelle ilianzia nchini Ghana, Afrika magharibi mwishoni mwa Juma . Katika mji mkuu Accra, Waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani alisema alizungumzia suala la Mali akisema Ujerumani iko tayari kuchangia wanajeshi katika shughuli za kusimamia amani za Umoja wa mataifa.

Waziri Westerwelle alisema bunge la Ujerumani litakuwa na usemi wa mwisho kuhusu suala hilo.

Ndege ya kijeshi ya kijerumani ikisaidia operesheni nchini Mali
Ndege ya kijeshi ya kijerumani ikisaidia operesheni nchini MaliPicha: Bundeswehr

Akigusia kuhusu kushiriki kwa Ujerumani katika mgogoro wa Mali, alisema kwamba hatua mbili za awali za mchango wa wanajeshi wa Ujerumani katika taifa hilo la Afrika magharibi, ziliwahusisha karibu wanajeshi 330 na hasa katika kusaidia mkakati wa kijeshi na pia mpango wa mafunzo uliogharimiwa na Umoja wa Ulaya .

Kikosi cha wanajeshi na polisi jumla ya 12,000 cha Umoja wa mataiafa kinatarajiwa kuchukuwa nafasi ya wanajeshi 6,000 wa nchi za kiafrika ifikapo mwezi Julai.

Kikosi cha Afrika kimekuwa kikisaidiwa na Ufaransa tangu mwaka jana na ambayo inaawahamisha wanajeshi wake 4,000 waliopelekwa Mali mwezi januari kupambana na makundi ya waislamu wa itikadi kali waliolitwaa eneo la Kaskazini la nchi hiyo.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, afp,rtr,dpa

Mhariri: Daniel, Gakuba