1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO kujadili kitisho cha UVIKO-19

4 Mei 2023

Kamati ya dharura ya shirika la Afya Duniani inakutana leo kujadili ikiwa virusi vya UVIKO-19 bado ni dharura ya kiafya ulimwengu.

https://p.dw.com/p/4QuXY
Umbo la Kirusi
Umbo la Kirusi Picha: DW

Mkutano huo unajiri zaidi ya miaka mitatu tangu kamati hiyoilipotangaza tahadhari ya juu zaidi ya shirika la Afya duniani kuhusu mripuko wa virusi vya UVIKO vilivyoanzia China.

Haijajulikana wazi wataalam wa kamati hiyo wataegemea upande upi. Lakini katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na baadhi ya ishara kwamba shirika la Afya Duniani liko wazi kutangaza mwisho wa dharura ya afya kutokana na UVIKO.

Wiki iliyopita, shirika la WHO lilisema vifo kutokana na UVIKO-19 vimepungua kwa asilimia 95 tangu mwanzo wa mwaka, lakini lilitahadharisha kwamba virusi hivyo bado vinasambaa.