Wieczorek-Zeul anaonya dhidi ya kupunguzwa misaada ya maendeleo
11 Oktoba 2008Matangazo
Washington:
Waziri wa misaada ya maendeleo wa serikali kuu ya Ujerumani bibi HeidemarieWieczorek-Zeul ameyaonya mataifa tajiri kiviwanda,mzozo wa fedha usije ukawa sababu ya kupunguzwa misaada kwa nchi maskini."Ni kwa masilahi ya nchi tajiri kiviwanda,ikiwa utaepukwa mwanya unaoigawa dunia sehemu mbili-masikini na matajiri-" amesema waziri huyo wa kutoka chama cha Social Democratic,mjini Washington."Hali kama hiyo itazidi kuchochea mizozo ambayo itazigharimu fedha nyingi zaidi nchi tajiri kuliko misaada yao ya maendeleo.Waziri Heidemarie Wieczorek-Zeul anategemea serikali kuu ya Ujerumani itatoa misaada ya maendeleo kama ilivyoahidi, licha ya mzozo wa fedha.Waziri Wieczorek Zeul alikua Washington kuhudhuria mkutano wa benki kuu ya dunia.