1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WIESBADEN : Watuhumiwa magaidi wa Kijerumani mbaroni

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpK

Mkuu wa Polisi wa Uhalifu wa serikali ya shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani amesema Wajerumani watatu wenye itikadi kali za Kiislam wenye nia ya kuanzisha mashambulizi nchini Ujerumani wamekamatwa nchini Pakistan.

Jörg Ziercke amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Wiesbaden nchini Ujerumani kwamba watu hao watatu ni miongoni mwa kundi la Wajerumani 10 wa itikadi kali za Kiislam ambao wamepatiwa mafunzo na wanamgambo wa Taliban kufanya mashambulizi ya kujitolea muhanga kwa kujiripua ndani ya Ujerumani pamoja na kuwaripua wanajeshi wa jeshi la Ujerumani wanaotumika nchini Afghanistan.

Amewaelezea wanaume hao watatu kuwa ni vijana raia wa Kijerumani waliobadili dini na kuwa Waislamu.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schaüble ameonya kwamba Ujerumani inakabiliwa na ongezeko la tishio la kigaidi na miongoni mwa tahadhari inazochukuwa ni kuchunguza mawasiliano ya kompyuta binafsi kupitia mtandao.

Schäuble amesema ni jambo lisiloepukika kabisa na itakuwa ni kinyume kwa kutowajibika kabisa kwamba kutotumia vifungu na vikomo vya mchakato wa sheria kujaribu kuchunguza njia za mawasiliano.

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Ujerumani pia ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Berlin juu ya kwamba wizara yake haina ushahidi madhubuti wa njama hizo za kigaidi udhibiti wa mipakani na hatua nyengine za usalama zimeimarishwa.