1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wiesinger achukua mikoba ya kuongoza Nuremberg

24 Desemba 2012

FC Nuremberg have named Michael Wiesinger to lead the team into the second half of the Bundesliga season. The move came just days after former coach Dieter Hecking left for Wolfsburg.

https://p.dw.com/p/178Yz
FUSSBALL Regionalliga Sued SAISON 2011/2012 18. Spieltag 20.11.2011 FC Bayern Muenchen II - 1. FC Nuernberg II Trainer Michael Wiesinger (1. FC Nuernberg II) Foto: Pressefoto ULMER/Claus Cremer xxNOxMODELxRELEASExx
Michael WiesingerPicha: picture alliance/Pressefoto Ulmer/Claus Cremer

Klabu ya FC Nuremberg imemteuwa Michael Wiesinger kuwa kaimu mkufunzi wake atakayeiongoza klabu hiyo hadi mwishoni mwa awamu ya pili ya msimu wa Bundesliga. Hatua hiyo inakuja baada ya Dieter Hecking kuihama klabu hiyo na kuchukua usukani katika klabu hasimu ya Wolfsburg kama kcoha.

Wolfsburg imesema Hecking amekubali mkataba wa hadi mwaka wa 2016. Hecking anachukua viatu vya Lorenz Guenther Koestner aliyejiuzulu Alhamisi wiki iliyopita baada ya kuhudumu kwa mara ya pili kama kaimu kocha. Koestner aliwaongoza Wolfsburg kutoka chini kabisa ya msimamo wa ligi hadi katika nafasi ya 12 na hadi katika robo fainali ya kombe la Shirikisho DVB Pokal, baada ya kuchukua usukani kufuatia kuondoka kwa Felix Magath Oktoba 25. Nuremberg iko pointi moja mbnele ya Wolfsburg katika Bundesliga.

Dieter Hecking ahamia Nuremberg
Dieter Hecking ahamia NurembergPicha: picture-alliance/dpa

Huntelaar atia saini Schalke

Mshambuliaji mahiri wa klabu ya Schalke 04 Mholanzi Klaas-Jan Huntelaar ameurefusha mkataba wake kwa miaka miwili hadi mwaka wa 2015. Huntelaar amesema amewaza kuhusu uamuzi huo kwa muda mrefu na sasa ana furaha wkamba maafisa wa klabu hiyo ya bundesliga wamemkubalia kuurefusha mkataba wake. Habari hizo ni nzuri kwa mkufunzi wa Schalke Jens Keller ambaye alipandishwa cheo kutoka wadhifa wa kuwa kocha wa timu ya vijana wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Huub Stevens aliyepigwa kalamu. Keller atashikilia hadi mwisho wa msimu. Schalke ambao walimaliza wa kwanza katika kundi lao la ligi ya mabingwa Ulaya, wamekuwa wakiyumbayumba nyumbani kwa kuzabwa mara nne na kutoshinda mchuano wowote katika mechi zao sita za mwisho, na kuwaacha wakiwa katika nafasi ya saba ya Ligi, pointi 17 nyuma ya viongozi Bayern Munich. Watasafiri Uturuki kwa mchuano wa mkondo wa kwanza wa awamu ya mwondowano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Galatasaray mnamo Februari 20. mchuano wa mkondo wa pili utakuwa katika uwanja wao wa Gelsenkirchen mnamo Machi 12.

Mbio za farasi wawili Uingereza

Kule Uingereza, nusu ya kwanza ya msimu wa Premier League imekamilika huku kukianza ratiba ya kitamaduni ya siku kuu ya Boxing Day, wakati Manchester United na Manchester City wote wakionekana kukusanya pointi nyingi katika kipindi hiki cha sherehe.

Manchester United wanalenga msimu huu kutwaa taji lao la 20
Manchester United wanalenga msimu huu kutwaa taji lao la 20Picha: AP

United, pointi nne kileleni mbele ya City, watakuwa na matumaini ya kuwazaba Newcastle wanaoyumbayumba, wakati mabingwa City wakisafiri kuchuana na Sunderland wakifahamu fika kwamba hawawezi kutaka kuteleza hata kidogo. Huku kukiwa na pointi saba zinazowatenganisha City na Chelsea katika nafasi ya tatu, taji tayari linaonekana kuwa mbio za farasi wawili, hata wakati kukiwa bado na mechi 20 msimu kukamilika. Lakini timu zote za mbili za Manchester zinafahamu kwamba hazifai kulegea na United inafaa kuwa chonjo baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Swansea jana Jumapili. Baada ya kungoja hadi dakika za majeruhi ili kuwashinda Reading goli moja kwa sifuri, City watataraji kupumua watakapotana na Sunderland. Chelsea bada ya kunyunyiza magoli manane kwa sifuri katika lango la Aston Villa wanasafiri nyumbani kwa Norwich wakitaraji kuendeleza matokeo hayo mazuri. Timu nne Arsenal. Everton, Tottenham na West Bromwich Albion zinatoshana pointi katika nafasi ya nne tano sita na saba lakini mchuano wa Arsenal umeharishwa kutokana na mgomo wa treni London. Everton watacheza na Wigan, wakati Tottenham wacheza ugenini dhidi ya Aston Villa nao West Brom wakipimana nguvu na Queens Park Rangers. Liverpool watachuana na Stoke City wakati Reading ikipambana na Swansea nayo Fulham ikichuana na Southampton.

Chuma cha Mourinho ki motoni

Nchini Uhispania, Kichapo dhidi ya Malaga Jumamosi bila shaka kimeyazika kabisa matumaini yoyote ya Real Madrid ya kutetea taji lao la La Liga na sasa wanahitaji kwa dharura kupata ufumbuzi ya matokeo yao mabaya, kabla ya kukutana na Manchester United katika Ligi ya Mabingwa tarehe 12 Februari.

Jose Mourinho ni lazima atafute suluhisho haraka iwezekanavyo
Jose Mourinho ni lazima atafute suluhisho haraka iwezekanavyoPicha: AP

Uamuzi wa mkufunzi Jose mourinho kumwacha nje kipa wake nambari moja ambaye ni nahodha mwenye ushawishi mkubwa kikosini Ikwr Casillas, katika mchuano huo ambao walizabwa magoli matatu kwa mawili, bado unazusha hisia za mshangao na sasa umewacha timu hiyo kuwa na pengo kubwa nyuma ya Barcelona.

Wako pointi 16 nyuma ya viongozi hao ambao hawajashindwa mechi hata moja Barca, baada ya mechi 17 na pointi saba nyuna ya nambari mbili Atletico Madrid. Mourinho aliutetea uamuzi wake wa kumweka benchi kipa wake Casillas akidokeza kwamba mlinda lango nambari mbili ambaye hana ujuzi wa kutosha Antonio Adan alikuwa katika hali nzuri kumliko Casillas mwenye umri wa mika 31, ambaye amekuwa katika lango la Madrid kwa mwongo mmoja na kuwa mpenzi wa mashabiki.

Mwandishi: Bruce Amani/reuters/AFP/DPA

Mhariri: Josephat Charo