1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WINDHOEK: China na Namibia kuimarisha uhusiano wa kibiashara

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUc

Rais Hu Jintao wa China akiendelea na ziara yake barani Afrika ametia saini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Namibia yenye utajiri mkubwa wa malighafi.Hata utalii kati ya nchi hizo mbili unatazamiwa kuimarishwa. Rais Hu vile vile ameahidi kuisaidia Namibia kujenga shule nchini humo.Leo,ziara ya Hu inampeleka Afrika ya Kusini,ambayo kibiashara barani Afrika,ni mshirika mkuu wa China.