1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WISCONSIN:Watu sita wauwawa kwa kupigwa risasi

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt1

Watu sita wameuwawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani.

Polisi wamekuta maiti za watu hao ndani ya numba moja katika mji mdogo wa Delavan.

Mtoto mdogo wa kike akiwa na umri wa kati ya miaka 2 na mitatu alikutikana akiwa amejeruhiwa vibaya ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba hiyo.Mtoto huyo yuko katika hali mahututi na amepelekwa hospitali kwa matibabu.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyotangazwa na kituo cha televisheni cha CNN tukio hilo linachukuliwa kuwa kitendo cha kujiua makusudi.