1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito wa kukomesha mapigano Ukanda wa Gaza

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cug8

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon kwa mara nyingine tena ametoa mwito wa kukomesha mapigano katika Ukanda wa Gaza.Ban amezikumbusha pande zote juu ya wajibu wa kuheshimu sheria ya kimataifa kuhusu binadamu na kutohatarisha maisha ya raia.Hasa ameeleza wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa Israel kufunga vituo vyote vya mpakani kati ya Gaza na Israel.

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon vile vile ametoa mwito kwa Israel kujizuia kuchukua hatua zitakazodhuru hali za umma wa kawaida katika eneo la Gaza.