1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliouwawa Gaza yapindukia 28,000

Amina Mjahid
10 Februari 2024

Wizara ya afya huko Gaza inayodhibitiwa na Hamas imesema zaidi ya watu 28,000 wameuwawa katika eneo hilo lililozingirwa tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi hilo la wanamgambo.

https://p.dw.com/p/4cFvB
Mapigano Gaza  | Khan Yunis
Idadi ya watu waliouwawa Gaza kufuatia vita vya Israel katika ukanda huo imefikia 28,000Picha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Idadi ya hivi karibuni ya waliouwawa imetokana na vifo vya watu 117 ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita. Taarifa ya wizara hiyo imesema watu wengine 67,611 wamejeruhiwa mjini Gaza tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7 mwaka jana. 

Wakati mapigano yakiendelea, jeshi la Israel limekuwa likisema linachukua hatua kuepuka mauaji ya raia katika operesheni yao wanayosema inawalenga wanamgambo wa Hamas. 

Iran: FIFA iipige marufuku Israel kufuatia mapigano Gaza

Hata hivyo Israel imekuwa ikikoseolewa kimataifa kufuatia idadi kubwa ya watu wanaouwawa katika mapigano hayo wakiwemo wanawake na watoto.