1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

wizi wa data Marekani.

26 Agosti 2008

Wasafiri nchini Marekani wajitolee kupekuliwa na hata kuibiwa data zao.

https://p.dw.com/p/F5FQ

Yule anaezuru Marekani,inambidi kujiweka tayari kupekuliwa.habari zake binafsi anabaidi kutaja,akubali kutia dole la shahada na mengi mengine.Kwani, tangu shambulio la kigaidi la septemba 11,2001 Idara ya usalama wa ndani ya marekani imekuwa ikizidi kufanya ukaguzi na msako wa aina hiyo.Jipya sasa msafiri anabidi kuruhusu kupekuliwa hata zana zake binafsi kama kama komputa za mkononi.

Wanabiashara wanaarifu kwamba katika Idara ya forodha wanapaswa kukaguliwa kwa muda wa hadi saa 1 Laptop zao na hawajui katika muda huo ni taarifa gani binafsi zinachukuliwa .

►◄

Amir Khan msafiri wa mara kwa mara anaelewa vyema visa kama hivyo: Kwani, kila mara muamerika huyu wa asili ya Pakistna anapowasili nyumbani Marekani kutoka ziara yake ya biashara barani ulaya,anabidi awakabnidhi maafisa walinzi wa mpakani wa Marekani komputa yake -laptop na awsatajie ufungo wsa kuingilia.

"Ukibisha,nitakuzuwia kupita -aliniambia afisa huyo wa ushuru wa forodha.Swali ,taarifa wanazochukua kutoka komputa yangu wanazifanya nini,hawataki kujibu.Hanisikilizi na huweka laptop yangu mahala ambapo siwezi kuiona."

Tim Gardner asema,

"Serikali mara moja ilitaifisha laptop yetu tunaporejea kutoka ngambo."

Mkasa huu umewahi pia kumpata Tim Gardner kutoka washington.Kupekuliwa mtu taarifa zake kunaweza kukadumu hadi masaa kadhaa.Hawajali iwapo ni taarifa za kibinafsi za banki au siri za kibiashara,iwapo ni barua ya mtu binafsi au ni picha alizopiga mtu likizoni-kila kitu maafisa wa mpakani wa Marekani waweza kukopi na kuzihifadhi katika komputa zao-asema Gardner.

Yule atakeificha ufungo wa kuingilia data zake katika komputa yake,atumai kuisamehe komputa yake hapewi tena.

Huu ni mtindo mbaya sana anadai David Cole,profesa wa sheria katika chuo kikuu cha Georgetown.

Kikundi cha wanabiashara wa kimarekani kilichokua safarini kimepeleka sasa mashtaka ya pamoja .Hadi hukumu kutolewa ,mtindo huu wa kupekuliwa wasafiri utaendelea. Nifanye nini auliza Amir Khan.

Siwezi kuachana na komputa yangu kwavile naihitajia kwa kazi zangu sawa na kipochi changu cha pesa.Zote mbili nazihitaji kila nendako.

kilio cha wasafiri hao hakisikizwi,kwani tangu hujuma ya septemba 11, 2001, Marekani inafanya ukaguzi mkali wa wasafiri.Anaetaka kuzuru Marekani,basi ajitolee uwanja wa ndege kujisabilia taarifa zake binafsi na kuzianika dhahiri-shahiri hadharani.Hii ni taarifa iliotolewa na Idaraza ya usalam wa ndani wa Marekani.Wamarekani wengi hawafurahishwi na desturi hii.Hasa polisi wa Marekani bila kukupa hoja yoyote au shaka shaka zozote hawana haki kwa muujibu wa sheria kuipekua nyumba yako -asema Marcia Hoffmann,wakili wa Umoja unaolinda taarifa za watu kutumiwa ovyo.