1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wladimir Klitschko astaafu mchezo wa ndondi

Bruce Amani
3 Agosti 2017

Bingwa wa zamani wa Ukraine wa ngumi za uzito wa juu Wladmir Klitschko ametangaza kustaafu kutoka mchezo wa ndondi. Anaondoka ulimwengu wa ndondi akiwa na rekodi ya ushindi katika mapigano 64 na kushindwa matano

https://p.dw.com/p/2hcVN
Wembley Boxen  Wladimir Klitschko vs Anthony Joshua
Picha: Getty Images

Klitschko anazitundika glovu zake akiwa mmoja wa wanamasumbwi nguli Zaidi wa muda wote ulingoni baada ya kutawala kwa kipindin cha miaka tisa na nusu akiwa bingwa wa uzito wa juu (heavyweight).

Pigano la mwisho la Mukraine huyo mwenye umri wa miaka 41 lilikuwa mwezi Aprili wakati aliangushwa na Anthony Joshua katika raundi ya 11 ya pigano lao la taji la WBA katika uwanja wa michezo wa Wembley mjini London.

"sikuwahi kufikiria ningekuwa na muda mrefu kama huu na kuwa na taaluma yenye mafanikio katika mchezo wa ndondi, nnawashukuru kutoka ndani ya moyo wangu", aliwaambia mashabiki wake kupitia taarifa.

"nimefanikiwa kupata kila kitu nilichokuwa nikikiota, na sasa nataka kuanza taaluma yangu ya pili baada ya michezo," alisema Klitschko.

Kustaafu kwake kunazima pigano kubwa lililotarajiwa kuandaliwa la marudiano kati yake na Joshua ambapo kulikuwa na uwezekano wa kuwa mjini Las Vegas.

Klitschko, ambaye alishinda dhahabu ya ngumi za uzito wa super heavy weight katika Michezo ya Olimpiki ya 1996, alishikilia taji la pamoja la mashirika ya ndondi kuanzia 2006-2015kabla ya kuchapwa na Tyson Fury mwaka wa 2015. Anaondoka ulimwengu wa ndondi akiwa na rekodi ya ushindi katika mapigano 64 na kushindwa matano

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo