1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfsburg kujihakikishia nafasi ya pili katika Bundesliga

Admin.WagnerD16 Mei 2015

Macho barani Ulaya yataelekezwa katika mchezo wa majaribio wa kombe la shirikisho nchini Ujerumani leo Jumamosi kati ya VFL Wolfsburg na Borussia Dortmund .

https://p.dw.com/p/1FQX9
Fußball Bundesliga 32. Spieltag SC Paderborn vs. VfL Wolfsburg
Wachezaji wa VFL Wolfsburg wakishangiria baoPicha: Getty Images/Bongarts/C. Koepsel

Wolfsburg na Borussia Dortmund iliyoko katika nafasi ya saba ya ligi ya Ujerumani Bundesliga zinapambana katika fainali ya kombe la Ujerumani DFB Pokal mjini Berlin Mei 30 lakini timu zote hizo zina vibarua ambavyo havijamalizika katika bundesliga.

Dortmund ambayo itampoteza kocha wao Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu , imepanda nafasi 11 , hadi nafasi ya saba tangu mapumziko ya majira ya baridi na ushindi utakuwa muhimu kwa timu hiyo katika juhudi zake za kujipatia nafasi katika kinyang'anyiro cha michuano ya Ulaya katika Ligi ya Europa.

Fußball Bundesliga 32. Spieltag SC Paderborn vs. VfL Wolfsburg
Mlinzi Naldo wa Wolfsburg akishangiria pamoja na mlinzi mwenzake Timm KlosePicha: picture alliance/dpa/J. Güttler

Kwa sasa Borussia iko pointi mbili nyuma ya mahasimu wao wakubwa Schalke 04 ambayo iko nafasi ya sita. Klopp amesisitiza vipi Wolfsburg imeweza kupata pointi tatu tu zaidi ya Dortmund tangu mapumziko ya majira ya baridi.

"Tofauti kati ya timu hizo mbili sio kubwa kama ilivyokuwa katika sehemu ya kwanza ya msimu huu, " amesema kocha wa Borussia Jurgen Klopp ambaye amesisitiza kuwa pambano la kombe la Ujerumani litakuwa pambano tofauti kabisa. Wolfsburg pia inahitaji ushindi ili kubakia mbele ya Borussia Moenchengladbach katika kuwania nafasi ya pili ya msimamo wa ligi katika Bundesliga. Na timu hiyo haijapoteza mchezo nyumbani msimu huu.

Marcel Schafer, Luiz Gustavo na Ivan Perisic wanatibiwa baada ya kupata mauamivu kidogo, lakini kocha Dieter Hecking amesema , " nia yetu ni kumaliza msimu huu bila ya kufungwa katika uwanja wa nyumbani." Borussia Moenchengladbach ambayo iko nafasi ya tatu , pointi mbili tu nyuma ya Wolfsburg , inakwenda mjini Bremen kupambana na Werder Bremen ikiwania ushindi wake wa kwanza mjini humo katika muda wa miaka 28.

Bayern yataka kulinda hadhi

Bado ikiwa katika maumivu ya kutolewa katika kinyang'anyiro cha kombe la mabingwa barani Ulaya katika nusu fainali na Barcelona, mabingwa Bayern Munich wanakaribishwa na Freiburg wakati kikosi hicho cha Pep Guardiola kinacheza tu kwa kulinda hadhi baada ya kunyakua ubingwa tayari wiki iliyopita

Wakati Schalke 04 ikiipumuliwa shingoni Borussia Dortmund inaikaribisha Parderborn inayokabiliwa na hatari ya kushuka daraja na imefanyia mageuzi kikosi chake baada ya mchezaji wa kati wa Ghana Kevin-Prince Boateng na mshambuliaji wa timu ya taifa ya ujerumani Sidney Sam kufutwa kutoka katika kikosi hicho

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Josephat Charo